Maafisa wa DCI Waokoa Mtoto wa miaka 4 baada ya Kutekwa nyara na mfanyakazi Murang'a

Muhtasari
  • Maafisa wa Upelelezi Waokoa Mtoto wa miaka 4 Kutekwa na mfanyakazi
  • Mtoto Liam alipatikana katika nyumba moja huko Naivasha, kufuatia siku kadhaa za utaftaji
Image: DCI

Wapelelezi wa Ofisi ya Utafiti wa Uhalifu na Upelelezi kwa kushirikiana na wale kutoka Kitengo cha Huduma Maalum (SSU) wamemuokoa mtoto wa miaka 4 aliyepotea mnamo Juni 2.

Mtoto Liam Ngucwa Mwangi alishukiwa kuchukuliwa na mfanyakazi wa nyanya yake, Charles King’ori maarufu  Delvin Maina, huko Murang’a.

Mtoto Liam alipatikana katika nyumba moja huko Naivasha, kufuatia siku kadhaa za utaftaji.

"Mtoto Liam Ngucwa Mwangi, ambaye alipotea Juni 2 huko Murang’a, leo mchana ameokolewa na wapelelezi wa DCI

Mtoto Liam ambaye anaaminika kutekwa nyara na mfanyakazi wa kiume wa nyanya yake, alipatikana katika nyumba moja huko Naivasha, kufuatia siku kadhaa za utaftaji wake mwingi," DCI Ilisema.

Makachero bado wanatafuta watekaji wa mtoto Liam ambao walitoroka muda mfupi kabla ya uokoaji.

"Uokoaji wa leo ulifuata ujumbe wenye uangalifu, uliotekelezwa na upelelezi kutoka Ofisi ya Utafiti wa Uhalifu na Ujasusi, iliyoongezwa na wenzao wa Kitengo cha Huduma Maalum. Wakati huo huo, wapelelezi wanawafuata watekaji wa Liam , ambao walitoroka muda mfupi kabla ya uokoaji.,"