logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mama aliyeenda kulalamikia gavana Waiguru apigwa mangumi na mlinzi

Kabla ya tukio hilo kuibuka, mama huyo ambaye alionekana kuwa na ujasiri mwingi alikuwa akieleza gavana Waiguru kuhusu mashinda zinazokumba wakazi wa wadi ya Kangai

image
na Radio Jambo

Burudani10 June 2021 - 21:07

Muhtasari


•Imeripotiwa kuwa mpiga kura huyo  aliyetambulishwa kama Damaris alikuwa analalamikia ugamvi duni wa rasilimali katika Kaunti ya Kirinyaga.

•Walinzi wa gavana walikuwa walikuwa wanamzuia mwanamke huyo kufikia Gavana kwani alionekana akikaribia gari lake kwa hasira.

Mama akieleza malalamiko kwa gavana Waiguru

Hasira imeelekezwa kwa Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi Waiguru baada ya video inayoonyesha mmoja wa walinzi wake akipiga mwanamke.

Kwenye video hiyo, mwanamke anayesikika akitoa malalamiko kwa gavana Waiguru anaonekana kupigwa mangumi na mmoja wa mlinzi wakati anajaribu kukaribia gari la gavana.

Imeripotiwa kuwa mpiga kura huyo  aliyetambulishwa kama Damaris alikuwa analalamikia ugamvi duni wa rasilimali katika Kaunti ya Kirinyaga.

“Sio pesa nataka mimi, nimejitafutia zangu tayari. Mbona wananisukuma na hatahawapigi kura? Huyu hapa hata labda hana kura ya Kirinyaga(akionyesha mmoja wa walinzi wa gavana}” Mama huyo anasikika akilalamika kudhulumiwa na walinzi wa gavana kabla ya mmoja wao kumvamia kwa mangumi.

Walinzi wa gavana walikuwa walikuwa wanamzuia mwanamke huyo kufikia Gavana kwani alionekana akikaribia gari lake kwa hasira.

Mwanamke huyo aliendelea kusisitiza kuwa sio pesa alitaka kumuomba gavana ila alitaka kueleza malalamiko yake  huku raia waliokuwa wanashuhudia tukio hilo wakijaribu kutenganisha wawili hao.

Kabla ya tukio hilo kuibuka, mama huyo ambaye alionekana kuwa na ujasiri mwingi  alikuwa akieleza gavana Waiguru kuhusu mashinda zinazokumba wakazi wa Kangai

Tumeishio kukutafuta ila hatujawahi kuona. Mungu ni mwema nikikuwa natoka shambani nikaambiwa kuwa unafunza huku. Nilipata na vijana hawa pande za Kagio nikawaambia tuandamane hapa tueleze mashida zetu kwako kwani tutakufa pande hii ya Kangai kwa sababu ya mashida” Mama huyo alisikika akiambia gavana.

“Sisi hatujui mambo ya samaki, wewe unafunza kuhusu samaki. Hatujui mambo ya kuku, hayo ndo unafunza. Mtu wa Mungu ni kuongea. Tunakupenda sana” aliendelea kusema.

Alilalimika kuwa hakuna kituo cha afya katika wadi ya Kangai na kuwa waliteseka sana kupata matibabu.

Gavana Waiguru alikuwa ameenda kuzindua mradi wa kufuga samaki unaotazamiwa kuongeza ukulima wa samaki katika Kaunti hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved