Faraja baada ya mwanamke aliyetekwa nyara Eastleigh kupatikana akiwa hai

Imeripotiwa kuwa Hafsa alipatikana ndani ya tanki ndogo la maji ambamo alikuwa amelazimishwa kutoshea, mshukiwa mmoja amekamatwa

Muhtasari

•Hafsa Mohamed, 23, alipatika katika chumba kilichotelekezwa maeneo ya Matopeni, Kayole kulingana na ujumbe uliotolewa na familia yake na polisi.

•Video ya kuhofisha ilienea mitandaoni ikionyesha mwanamke aliyeaminika kuwa Hafsa akiteswa na watu ambao hawakuwa wanajioyesha kwa kamera. Mhasiriwa ambaye alikuwa amefungwa macho  alionekana kuwa na majeraha usoni.

Hafsa Mohamed
Hafsa Mohamed
Image: Hisani

Hatimaye mwanamke wa asili ya Kisomali ambaye alitekwa nyara Juni 14 ameokolewa na maafisa wa polisi.

Hafsa Mohamed, 23, alipatika katika chumba kilichotelekezwa maeneo ya Matopeni, Kayole kulingana na ujumbe uliotolewa na familia yake na polisi.

Polisi wameeleza kuwa mhasiriwa alipatikana akiwa peke yake wakati alipookolewa kwani waliokuwa wamemteka nyara walikuwa wameondoka.

Imeripotiwa alipatikana ndani ya tanki ndogo la maji  ambamo alikuwa amelazimishwa kutoshea.

Punde baada ya kuokolewa, Hafsa alipelekwa katika kituo cha polisi kabla ya kufikishwa hospitalini kwa ukaguzi wa kidaktari. 

Familia ya Hafsa imethibitisha kuwa hakuna malipo yoyote ambayo walikuwa wametumia wahalifu hao licha ya kuagizwa kulipa shilingi milioni 5.

Polisi wameeleza kuwa eneo ambalo  mwanamke huyo alipatikana ni moja ya maeneo ambayo walikuwa wanaangazia sana. Hata hivyo, haijaeleweka mbona watekaji nyara wale waliamua kumuacha kwenye chumba hicho .

Kufuatia hayo, mshukiwa mmoja, mwanaume wa miaka 24 anayeaminika kuwa mmoja wa kikundi cha magaidi ambao walimteka nyara Hafsa amekamatwa na anaendelea kuhojiwa na wapelelezi wa DCI. 

Hafsa alitekwa nyara siku ya Jumatatu katika maeneo ya Kamukunji na familia yake ikaeneza habari mitandaoni kuwa alikuwa amepotea.

Camera ya CCTV ilikuwa imerekodi mara ya mwisho Hafsa alipoonekana katika duka la nguo mida ya saa kumi na moja jioni.

Siku chache baadae, familia ya Hafsa ilianza kupokea video na jumbe kutoka kwa watekaji nyara waliokuwa wamemkamata huku wakidai kulipwa  Ksh 5M ili wamuachilie

"Nimeshikwa na wanataka pesa tafadhali mtume" Mhasiriwa ambaye alionekana kuwa mwenye hofu alisika kusema kwenye video moja iliyokuwa inaenea mitandaoni.

Sauti ya mwanaume iliwanga inasikika ikimpea masharti.

Inadaiwa kuwa watekaji nyara wale walitumia familia ya Hafsa video hiyo pamoja na zingine huku wakidai kulipwa Sh5M.

Video hizo zilifuatwa na jumbe kadhaa  za watekaji nyara hao wakidai kulipwa.

Familia ilipiga ripoti katika kituo cha California, Eastleigh tarehe 15  mwezi huu wa Juni.

Maafisa wa polisi wamesema kuwa watekaji nyara wamekuwa wakihama kwenda maeneo mbalimbali ili kuepuka kupatikana