Marufuku ya kutosafiri usiku kuondolewa ili kukwamua uchumi

Muhtasari

• Madereva wa mabasi ya abiria ya masafa marefu wameirai serikali kuondoa marufuku ya kutosafiri usiku.

Waziri wa Uchukuzi Jmes Macharia

Madereva wa mabasi ya abiria ya masafa marefu wameirai serikali kuondoa marufuku ya kutosafiri usiku.

Madereva hao na wadau wengine siku ya Alhamisi walitaka serikali kulegeza baadhi ya kanuni za kudhibiti maambukizi wa virusi vya Corona.

Walisema baadhi ya kanuni hizo zimehujumu sana mikakati ya kukwamua uzorotaji wa uchumi wa taifa.

Janga la Corona limedidimiza malengo ya ukuaji wa uchumi kwa zaidi asilimia 10 na kutoka ukuaji wa asilimia 6 sasa uchumi umedorora hadi ukuaji wa sasa wa asilimia chini ya moja.

Wakiongozwa na mkurugenzi wa mabasi ya uchukuzi ya Masha mjini Voi Zaid Farouk, Wahudumu wa uchukuzi wa masafa marefu wanasema licha ya kuruhusiwa kubeba abiria kwa kiwango cha kawaida, wakenya wengi wangali wanakabiliwa na changamoto ya kusafiri kutokana na marufuku ya kutosafiri usiku.

Wakati huo huo, Uvamizi wa ndovu katika maeneo mengi ya wakaazi katika kaunti ya Taita Taveta umetajwa kama changamoto kuu ya serikali ya kaunti kuunganisha maji safi kwa wenyeji.

Waziri wa maji Esther Mwanyumba amelaumu shirika la KWS kwa kuzembea kazini huku ndovu wakipasua matangi ya maji maeneo katika maneo mbalibali  ya kaunti hiyo.

Sawia na maeneo kadhaa nchini, kaunti ya Taita Taveta inakabiliwa na kiangazi huku baadhi ya wakaazi wakihitaji misaada ya chakula na maji.