rais Kenyatta atetea mfumo ya CBC

Utoaji wa kitaifa wa CBC ulianza Januari 2019 katika chekechea na gredi ya I na II na darasa la 1, 2 na 3.

Muhtasari

• Rais alisema CBC, ambayo ni moja ya mafanikio yake makubwa, inakusudia kuandaa nchi hiyo ili itoe kazi nzuri na ubunifu.

CBC
CBC
Image: HISANI

Rais Uhuru Kenyatta ametetea mtaala mpya wa CBC  akisema utaongeza ushindani n ubunifu.

Wazazi wengi na wadau wengine wamekuwa wakilalamikia mtaala wa CBC wakisema kwamba mtaala huo umeongozea wazazi kazi nyingi na gharama kwa wazazi, wengi wao wakikosa wakati na pesa vinavyohitajika kufanikisha mtaala huo.

"Pia tumewasilisha mtaala wa kitaifa unaozingatia uwezo na ufikiaji wa masomo kwa wote, ambao utazidisha ushindani wa wafanyikazi wetu," Uhuru alisema wakati wa kikao cha 76 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jumatano.

Rais alisema CBC, ambayo ni moja ya mafanikio yake makubwa, inakusudia kuandaa nchi hiyo ili itoe kazi nzuri na ubunifu.

"Tunatekeleza mipango kabambe ya kuandaa nchi ... Uwekezaji wetu katika barabara, miundombinu ya anga na bandari, na vituo muhimu vya huduma za afya nchini kote, ni kubwa zaidi na ya kutamani katika historia yetu," alisema.

"Kenya imebarikiwa kuwa na vijana, wenye elimu nzuri, na wenye tija ambao wameweza kujenga moja ya nchi zenye uchumi mchanganyiko barani Afrika."

Mzazi mmoja amewasilisha kesi mahakamani akitaka kusitisha utekelezaji zaidi wa Mtaala wa CBC ambao tayari unatekelezwa katika shule za msingi.

Esther Ang’awa, ambaye pia ni wakili wa Mahakama Kuu, anasema CBC imeweka mzigo wa kiuchumi kwa watoto, walimu, wazazi na walezi.

Utoaji wa kitaifa wa CBC ulianza Januari 2019 katika chekechea na gredi ya I na II na darasa la 1, 2 na 3.

Mtaala wa 2-6-3-3-3 ulipendekezwa kama mfumo unaohitajika kukwamua nchi na kuziba mianya inayoachwa na mtaala wa 8-4-4.