Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed amejipata taabani kufuatia matamshi tatanishi ambayo alitoa hadharani siku ya Ijumaa.
Junet amekosolewa sana mitandaoni kuhusiana na madai yake kwamba iwapo Raila Odinga atanyakua kiti cha Urais kwenye chaguzi kuu za mwaka ujao basi serikali itakuwa mikononi mwa wakazi wa eneo la Nyanza.
Alipokuwa anatoa hotuba yake kwenye hafla ya kuchanga pesa iliyofanyika katika kaunti ya Nyamira ambayo ilikuwa imehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Raila Odinga, waziri Fred Matiang'i na Mutahi Kagwe, Junet alisikika akihakikishia wakazi kwamba uongozi utakuwa wao iwapo kinara wa ODM atachukua usukani kutoka kwa rais Uhuru Kenyatta.
Junet alimuomba waziri wa afya Mutahi Kagwe asikasirishwe na matamshi yake huku akidai kwamba eneo alilotoka la Mlima Kenya limekuwa likitawala kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini.
"Hapa Nyanza sisi ni watu moja, sisi ni jamii moja. Tusiwe na wasiwasi. Baba akishinda, serikali ni yetu watu wa Nyanza, Sitaki watu wa gazeti wasikie hiyo, Mutahi Kagwe anaweza kasirika, lakini ata nyinyi mlikuwa nayo miaka ishirini na kadharika. Safari hii ni yetu watu wa Nyanza. Mutahi utakuja hapa kama mgeni" Junet alisema.
Matamshi ya mwanasiasa huyo hata hivyo hayajapokewa vyema haswa na wafuasi wa mpinzani mkubwa wa Raila Odinga, naibu rais William Ruto.
Mbunge wa eneo la Soy Caleb Koistany ni miongoni mwa Wakenya waliokuwa katika mstari wa mbele kusuta matamshi ya Junet.
If Raila wins, the government will be for us Nyanza people says Junet .
— Hon Caleb Kositany MP Soy (@ckositany) October 23, 2021
Hustler nation is for all Kenyans.
@JunetMohamed pic.twitter.com/1CjqO4ld7E
Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungw'a alisisitiza kwamba Junet alikuwa anazungumza yaliyokuwa moyoni mwake huku akipuuzilia mbali azimio la kinara wa ODM la kuwa rais.
Good thing with my good friend .@JunetMohamed is honesty while speaking. He says it as it is,It’s all about political POWER and NOTHING more for them. No plan No Vision No Agenda. pic.twitter.com/Ifs5OyA40q
— KIMANI ICHUNG'WAH (@KIMANIICHUNGWAH) October 22, 2021
Junet Mohammed tells CS Mutahi Kagwe that Kikuyus won't be part of Raila's government. 😭😭 pic.twitter.com/5AUeymyifa
— Mukami Wa Embu 🇰🇪 (@MukamiWaEmbu) October 23, 2021
Imagine the likes of Junet being in the government of Raila. His utterance confirms other communities will have it rough. Raila's presidency will be biggest mistake to ever happen. I believe God has good reasons he has never allowed him president. Vote for him at your own peril
— Chebett (@KiruiChebet8) October 23, 2021
So after Mutahi Kagwe declared support to baba, Junet, Raila's most trusted ally, the ever present everywhere Raila is, Raila's confidant, told him the government they are going to form is theirs and Mutahi will be going there as a visitor. If I were Mutahi I'd have just left!
— WMM (@WMMartha) October 23, 2021
Mamia ya Wakenya wameendelea kutoa hisia mbalimbali mitandaoni wengine wakikemea matamshi ya mbunge huyo huku wengine wakimtetea kwamba yalikuwa ya kitani tu.