'Ni wazimu kuwa jamaa ataka kuniua pamoja na walio karibu nami juu amekataliwa!' Lilian Ng'anga asikitishwa na vitisho vya Mutua

Lilian amedai kuwa mapenzi yake ni watengane vizuri kama watu wazima

Muhtasari

•Kupitia ujumbe ambao alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram asubuhi ya Jumapili, Lilian amesema angependa kuwe na amani kati yake na gavana Mutua ila sio kisasi.

•Kulingana na mpenzi huyo wa Juliani, kitendo cha gavana  Mutua cha kutishia kumuua pamoja na walio karibu naye kwa sababu alimkataa ni kitendo cha kale.

•Lilian ameeleza uhusiano wake na mgombeji huyo wa kiti cha urais mwaka ujao ulivyokuwa huku akisisitiza hawakuwa mume na mke.

Image: INSTAGRAM// LILIAN NGANGA

Lilian Ng'anga ameendelea kuzungumza kuhusu masaibu yayiyofuata baada ya utengano wake na gavana wa Machakos  Alfred Mutua mapema mwaka huu.

Huku wawili hao wakionekana kuwa na uhusiano mbaya katika kipindi cha miezi michache iliyopita, Lilian amedai kuwa mapenzi yake ni watengane vizuri kama watu wazima.

Kupitia ujumbe ambao alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram asubuhi ya Jumapili, Lilian amesema angependa kuwe na amani kati yake na gavana Mutua ila sio kisasi.

"Mimi ningependa tuwe na utengano mzima na wenye urafiki. Ningependa amani kati yetu na mwishowe tuwe marafiki, baada ya yote tumekuwa pamoja kwa mwongo mmoja" Lilian amesema.

Kulingana na mpenzi huyo wa Juliani, kitendo cha gavana  Mutua cha kutishia kumuua pamoja na walio karibu naye kwa sababu alimkataa ni kitendo cha kale.

"Ni wazimu kuona mwanaume anataka kuniua na watu walio karibu nami kwa sababu nilisema HAPANA. Kitenda cha kale vipi!" Amesema Lilian.

Pia amefutulia mbali madai kuwa alisababisha kuvunjika kwa ndoa ya kwanza ya Mutua mwongo mmoja uliopita huku akieleza kwamba tayari ilikuwa imevunjika kitambo kabla hajajitosa kwenye mahusiano na gavana huyo.

Lilian ameeleza uhusiano wake na mgombeji huyo wa kiti cha urais mwaka ujao ulivyokuwa huku akisisitiza hawakuwa mume na mke.

"Alichokuwa amefanya Alfred ni "Kuhanda ithege" ikija kwa ndoa. Najua, naheshimu na kukubali kuwa kushirikiana kwaweza kuitwa ndoa lakini hatukuwahi tia saini kwenye karatasi zozote kuonyesha kuwa tulikuwa tumefunga ndoa kihalali.  Hatukufunya jambo lolote la kitamaduni ambalo lingetufanya mume na mke" Lilian ameeleza.

Amesema kuwa inasikitisha kuona wanawake wakidhalilishwa katika jamii huku akishinikiza watu kubali tamaduni hiyo.