Tanzia: Radi yaua mtoto Bungoma

Muhtasari

• Mwanafunzi wa darasa la Saba katika shule ya msingi ya Buema, katika kata ya Musikoma, eneo bunge la Kanduyi alifariki dunia baada ya kupigwa na radi siku ya Alhamisi. 

• Alikuwa amerejea kutoka shuleni na alikuwa akiwalisha sungura wake kisa hicho kilopotokea.

• Babake marehemu alisema mwanafunzi huyo alichuna mboga na kuanza kuwalisha sungura wake lakini kukatokea radi kali. 

Mwanafunzi wa shule ya msingi alifariki papo hapo katika Kaunti ya Bungoma baada ya kupigwa na radi. 

Mwanafunzi wa darasa la Saba katika shule ya msingi ya Buema, katika kata ya Musikoma, eneo bunge la Kanduyi alifariki dunia baada ya kupigwa na radi siku ya Alhamisi. 

Alikuwa amerejea kutoka shuleni na alikuwa akiwalisha sungura wake kisa hicho kilopotokea.  Babake marehemu alisema mwanafunzi huyo alichuna mboga na kuanza kuwalisha sungura wake lakini kukatokea radi kali. 

“Dada yake alitoka kwenda kumuita ili tupate chakula cha jioni pamoja lakini alimkuta amelala, jitihada za kumwamsha hazikufua dafu kwani hakuitikia,” alisema.

 Alikimbizwa hospitali lakini alikuwa tayari amefariki. 

"Nimesikitishwa na kifo chake, alikuwa kijana mchapakazi ambaye nilikuwa na matumaini mengi sana kwake, sielewi nani ataziba pengo," alisema babake huku akitiririkwa. 

Visa vya vifo vya radi vimeongezeka eneo hilo jambo ambalo limelazimu shule kuweka vifaa vya kudhibiti radi.