logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa akamatwa baada ya kutekeleza wizi wa mabavu Shauri Moyo, wenzake watatu wasakwa

Otieno alipokuwa anatoroka kuokoa maisha yake alitoa kisu chake na kukata jirani yule kichwani kwa kuwaharibia 'sherehe' yao.

image
na Radio Jambo

Habari02 December 2021 - 02:33

Muhtasari


• Otieno alipokuwa anatoroka kuokoa maisha yake alitoa kisu chake na kukitumia kukata jirani yule kichwani kwa kuwaharibia 'sherehe' yao.

Crime scene photo

Polisi katika kaunti ya Nairobi wanazuilia mshukiwa mmoja wa wizi mabavu kufuatia tukio la ujambazi lililotokea katika nyumba moja mtaa wa Shauri Moyo.

Ian Otieno 25, na wenzake watatu walikuwa wamevamia nyumba ya familia katika eneo la Juakali mwendo wa saa nne usiku wa Jumanne na kuagiza wenye nyumba walale chini kabla ya kuiba simu tatu, runinga ya inchi 43 kati ya vitu vingine vya thamani.

Kwa bahati nzuri jirani mmoja aliwaona majambazi hao wakitishia familia ile na akaanza kupiga nduru ambayo iliwashtua wakaanza kutoroka.

Kulingana na DCI, Otieno alipokuwa anatoroka kuokoa maisha yake alitoa kisu chake na kukitumia kukata jirani yule kichwani kwa kuwaharibia 'sherehe' yao.

Mwenye nyumba iliyokuwa inavamiwa alipigia polisi kutoka kituo cha Shauri Moyo ambao walifuata genge lile na kuweza kumkamata Otieno akiwa bado amebeba televisheni ambayo  walikuwa wameiba.

Kisu kilichokuwa na damu kilipatikana kikiwa kimefichwa kwenye suruali yake.

Polisi wanaendelea kuwasaka wenzake Otieno huku akiwa anasubiri kufikishwa mahakamani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved