logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watanzania watawala orodha ya mchujo wa tuzo ya fasihi ya Kiswahili

Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika imetangaza majina ya wanaowania tuzo ya mwaka wa 2021.

image
na

Football03 December 2021 - 09:31

Muhtasari


• Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika imetangaza majina ya wanaowania tuzo ya mwaka wa 2021.

• Mchakato wa kutathmini zawadi za 2021 unafanywa na Prof. Aldin K. Mutembei, Dkt. Salma Omar na Dkt. Joseph Nyehita Maitaria.

• Washindi wa jumla watatangazwa katika hafla ya utoaji tuzo iliyopangwa kufanyika tarehe 27 Januari 2022 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mkuu wa Masoko, Kenya na Afrika Mashariki, wa Kampuni ya MRM Bw. Harry Njagi akihutubia mkutano, Desemba 2, 2021 wakati wa kutangaza walioteuliwa katika hoteli ya Nairobi.

Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika imetangaza majina ya wanaowania tuzo ya mwaka wa 2021.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell kwa Fasihi ya Afrika, Abdilatif Abdalla, alipokuwa akiwatangaza wateule hao alisema majaji wake walifanya zoezi kali la kuchagua orodha bora zaidi ya mchujo katika vitengo tofauti vya washiriki.

Alionyesha kuridhishwa na kiwango cha juu cha mawasilisho yanayothamini na kukuza fasihi ya Kiafrika.

Akizungumza siku ya Alhamisi wakati wa tangazo hilo katika hoteli moja mjini Nairobi, Abdilatif Abdalla alisema ubora wa kazi iliyowasilishwa na kuvunjwa kwa vizuizi vya kijiografia vya kazi ya fasihi nje ya mipaka ya Afrika ni kauli kali kwamba fasihi ya Kiafrika inaendelea kukua kwa kiasi kikubwa na kutambuliwa.

Mchakato wa kutathmini zawadi za 2021 unafanywa na Prof. Aldin K. Mutembei, Dkt. Salma Omar na Dkt. Joseph Nyehita Maitaria.

Kazi na waandishi walioteuliwa ni Ubunifu: Kirusi Kipya - Halfani Sudy (Tanzania), Bweni la Wasichana- Lucas Lubango (Tanzania) na Kido Kanzu ya Ukubwa -Hafidh Athumani (Tanzania); Ushairi: Chemchemi jangwani- Moh’d Omar Juma (Tanzania), Malenga wa Masasi - Msusa Mohamedi Msusa (Tanzania) na Sinaye Baba- Mfaume Hamisi Mfaume (Tanzania); Play: Sinaubi- Mbwana Kidato- Anaishi Afrika Kusini (Tanzania).

Washindi wa jumla watatangazwa katika hafla ya utoaji tuzo iliyopangwa kufanyika tarehe 27 Januari 2022 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Tuzo hiyo itatolewa kwa hati bora zaidi ambayo haijachapishwa au kitabu kilichochapishwa ndani ya miaka miwili ya mwaka wa tuzo katika vitengo vya hadithi za kubuni, ushairi na kumbukumbu, na riwaya za picha.

Jumla ya tuzo zilizopendekezwa za dola 15,000 za Kimarekani zitagawanywa kama tuzo ya 1 ya hadithi za kubuni/ hadithi halisi- $5,000, Mshindi wa Ushairi- $5,000 na Mshindi wa pili katika kila kitengo atapokea  $2,500.

Mbali na zawadi ya pesa hiyo, washiriki pia watazingatiwa kuchapishwa kwa kazi zao na East African Education Publishers nchini Kenya na Kiswahili by Mkuki na Nyota Publishers nchini Tanzania huku mashairi yatakayoshinda yatatafsiriwa kwa Kiingereza na Kuchapishwa na Africa Poetry Book Fund.

Tuzo hii inadhaminiwa na Mabati Rolling Mills ya Kenya, ALAF Tanzania, Ofisi ya Makamu Mkuu wa wa Masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Cornell, Kituo cha Mafunzo ya Africana katika Chuo Kikuu cha Cornell na Wakfu wa Ngugi wa Thiong’o.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved