Nyota wa mbio za mita 100 Ferdinand Omurwa Omanyala amejiunga na huduma ya polisi nchini (NPS).
NPS ilitangaza kwamba mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25 amechukua jukumu mpya ambalo litamfanya awakilishe sio taifa tu bali pia polisi katika mashindano yajayo.
Omanyala ambaye anashikilia rekodi ya Afrika katika mbio za mita 100 alifahamishwa kuhusu jukumu lake jipya alipoalikwa na inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambai katika ofisi yake iliyo Jogoo House siku ya Ijumaa.
Gwiji huyo sasa anajiunga na wanariadha wengine wanaowakilisha polisi kama vile David Rudisha, Geoffrey Kamworor, Vivian Cheruiyot, Julius Yego, Ezekiel Kemboi kati ya wengine wengi.
Akizungumzaa baada ya kukabidhiwa wadhfa huo, Omanyala alishukuru NPS na serikali kwa kusaidia katika ukuzaji wa talanta huku akiahidi matokeo bora katika mbio atakazokimbia.
"ni heshima kutumikia huduma ya polisi ya kitaifa na ninaahidi kujitolea kadri niwezavyo kama mwanariadha. Pia ninaelewa kuwa kuna maisha baada ya kukimbia" Omanyala alisema.
Voila! Ferdinand Omanyala Omurwa, Africa's 100m record holder and Kenya's sensational sprinter has joined the National Police Service. The 25-year-old athlete has taken up a new role that will see him represent the National Police Service and the country in future track events. pic.twitter.com/mTqM8jzUbe
— National Police Service-Kenya (@NPSOfficial_KE) December 3, 2021
Mutyambai alihimiza Omanyala adumishe nidhamu yake katika michezo ili aweze kupata mafanikio makubwa na aweze kutekeleza majukumu yake mapya kama mwanariadha wa polisi.
Mapemaa mwaka huu Omanyala aliandikisha rekodi mpya ya Afrika katika mbio za mita 100 baada ya kukimbia kwa sekunde 9.77 katika mashindano ya Kip-Keino yaliyofanyika katika ukumbi wa Moi, Kasarani mnamo Septemba 18.