Watu 18 wamethibitishwa kufariki huku wengine 10 wakiokolewa baada ya basi kuzama katika mto wa Enziu ulio eneo la Mwingi kaunti ya Kitui.
Kamanda wa polisi katika eneo hilo Joseph Yakan amesema basi hilo la shule ya Sekondari ya Mwingi Seminary lilikuwa limebeba abiria waliokuwa wanaenda kuhudhuria harusi.
Tukio hilo linaripotiwa kutokea mwendo wa saa tano asubuhi ya Jumamosi katika kijiji cha Ngue, wadi ya Nuu.
Basi hilo lilikuwa limebeba zaidi ya abiria 30 ambao wanasemekana kuwa wanakwaya kutoka kanisa la katoliki la Mwingi.
Katika video iliyoonekana na Radio Jambo, basi hilo lilikuwa linajaribu kuvuka daraja lililokuwa limefurika maji wakati mikondo ya maji yenye nguvu ililibeba na kulizamisha ndani ya mto.
Kilio na nduru kubwa kutoka kwa wanakijiji ambao walishuhudia zilitanda hewani katika eneo la tukio punde baada ya ajali hiyo ya kusikitisha kutokea. Magari mengine yalionekana kuhofia kuvuka daraja lile.
Few moments ago at Enziu River, these ones had dressed for some wedding event happening at Nuu Ward in Mwingi - Kitui County. I hope all of them got rescued. pic.twitter.com/o8XxiedF2q
— Kwale Gunner - #MadeInKenya 🇰🇪 (@Sam_Lulli) December 4, 2021
Yakan amesema kwa sasa basi hilo bado limezama kwenye matope huku akiongeza kuwa juhudi za uokoaji zinaendelea.
Inahofiwa huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka uokoaji unapoendelea kwani idadi halisi ya abiria waliokuwemo bado haijathibitishwa.
Mengi yanafuata...