logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Natembea ahamishwa kwa ofisi ya rais licha ya kutangaza kujiuzulu

Maeneo ya Nairobi na Bonde la Ufa yamepata wakuu wapya (RC) katika mabadiliko yaliyotangazwa na Ofisi ya Rais.

image
na Radio Jambo

Mahakama13 January 2022 - 06:52

Muhtasari


• Maeneo ya Nairobi na Bonde la Ufa yamepata wakuu wapya (RC) katika mabadiliko yaliyotangazwa na Ofisi ya Rais.

• Mabadiliko hayo yalitangazwa na Katibu wa kudumu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Karanja Kibicho ambaye alisema yatatekelezwa mara moja.

• Mkuu wa kanda ya Mashariki Isaiah Nakoru alihamishwa hadi Magharibi katika wadhifa sawa na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna wa Kaunti ya Narok Evans Achoki.

Mratibu wa Bonde la Ufa George Natembeya. Picha: JOSEPH KANGOGO

Maeneo ya Nairobi na Bonde la Ufa yamepata wakuu wapya (RC) katika mabadiliko yaliyotangazwa na Ofisi ya Rais.

Pia maeneo yalioathrika katika mabadiliko hayo ni Magharibi, Mashariki, Kati na Kaskazini Mashariki.

Mabadiliko hayo yalitangazwa na Katibu wa kudumu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Karanja Kibicho ambaye alisema yatatekelezwa mara moja.

Mkuu mpya wa eneo la Nairobi ni William Kangethe Thuku ambaye wiki mbili zilizopita aliteuliwa kuwa Katibu mwandamizi wa Utawala wa Huduma za Urekebishaji.

Mkuu mpya wa Bonde la Ufa atakuwa Kamishna wa Kaunti ya Makueni Mohamed Maalim.

Mabadiliko haya yanajiri siku moja baada ya George Natembeya kutangaza kujiuzulu wadhifa wake kama mkuu wa kanda ya Bonde la Ufa ili kuwania kiti cha gavana wa Kaunti ya Trans Nzoia.

Ingawa alingaza kujiuzulu siku ya Jumanne, kulingana na mabadiliko yaliyofanywa Natembeya amehamishwa hadi Harambee House ambapo anatarajiwa kukamisha utaratibu wake kujiuzulu.

Walioathiriwa waliagizwa kwenda katika ofisi ya Rais Harambee House na kufahamishwa kuhusu mabadiliko hayo.

Mkuu wa kanda ya Mashariki Isaiah Nakoru alihamishwa hadi Magharibi katika wadhifa sawa na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna wa Kaunti ya Narok Evans Achoki.

Mkuu wa kanda ya Magharibi Esther Maina alihamishwa hadi Kati katika wadhifa huohuo huku James Kianda wa Nairobi akitumwa Kaskazini Mashariki kuchukua nafasi ya Nicodemus Ndalana aliyerejeshwa Harambee House.

Mkuu wa kati Wilfred Nyagwanga alirejeshwa katika Harambee House. Mabadiliko hayo yanakuja kufuatia wito wa jinsi shughuli zinavyoendeshwa katika mikoa kabla ya uchaguzi wa Agosti.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved