logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Hayupo tena kwenye orodha ya jamaa zangu!" Atwoli amkana aliyekuwa mkewe baada ya kujiunga na UDA

Bi Roselinda alizinduliwa kama mwanachama mpya wa UDA katika ziara ya naibu rais ya eneo la Magharibi ambapo alihutubia wakazi na kujitambulisha kama mke wa Atwoli

image
na Radio Jambo

Habari29 January 2022 - 05:21

Muhtasari


•Bi Roselinda alizinduliwa kama mwanachama mpya wa UDA katika ziara ya naibu rais ya eneo la Magharibi ambapo alihutubia wakazi na kujitambulisha kama mke wa Atwoli

•Kwa sasa Atwoli ako kwenye ndoa na mtangazaji wa habari wa KTN Mary Kilobi baada ya kutengana na Bi Roselinda miaka kadhaa  iliyopita.

Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli

Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli amepuuzilia mbali mahusiano kati yake na  Bi Roselinda Simiyu ambaye alijitambulisha kama mke wake Ijumaa alipojiunga na UDA.

Bi Roselinda alizinduliwa kama mwanachama mpya wa UDA katika ziara ya naibu rais ya eneo la Magharibi ambapo alihutubia wakazi na kujitambulisha kama mke wa Atwoli

"Mimi naitwa Mama Roselinda Simiyu. Mzee wangu anaitwa Francis Atwoli na niko ndani, ndani ya Hustler!" Bi Roselinda alisema.

Ruto amkaribisha Bi Roselinda Simiyu jukwaani mnamo Ijumaa, Januari 28

Kufuatia hayo Atwoli alijitosa kwenye mitandaoni ya kijamii na kueleza kuwa walitengana na Bi Roselinda na hamtambui tena kama mwanafamilia wake.

Hali kadhalika bosi wa COTU alisisitiza kwamba eneo la Magharibi linaunga mkono muungano wa Azimio la Umoja huku akipatia  Ruto idhini ya kumchukua mke huyo wake wa zamani bila malipo.

"Roselinda alijisalimisha kwa William Ruto mnamo 2007 katika nyumba yake iliyo mjini Eldoret. Hayupo tena kwenye orodha ya jamaa zangu. Ruto sasa anaweza kumuongeza, bila malipo, kwa wake zake wawili wa ndevu aliowapata hivi majuzi ili awe na wake watatu kutoka magharibi. Eneo la Magharibi liko katika Azimio" Atwoli alisema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Kwa sasa Atwoli ako kwenye ndoa na mtangazaji wa habari wa KTN Mary Kilobi baada ya kutengana na Bi Roselinda miaka kadhaa  iliyopita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved