Wanga apewa tikiti ya moja kwa moja na ODM kuwania ugavana Homabay

Muhtasari

• Gladys Wanga ateuliwa kama mgombeaji wa ugavana kaunti ya Homabay kupitia tikiti ya ODM.

• Raila Odinga alisema uamuzi huo uliafikiwa baada ya mazungumzo ya kina na viongozi wa chama hicho.

Mwakilishi wa kina mama katika kaunti ya Homabay, Gladys Wanga amepewa tikiti ya moja kwa moja na chama cha ODM kuwania wadhfa wa ugavana katika kaunti hiyo.

Kupitia ujumbe uliotolewa na  kinara wa chama Raila Odinga, kulikuwa na wawaniaji wengine saba  ambao walilazimika kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho na kumuunga mkono Wanga.

Aidha, mheshimiwa Oyugi Magwanga aliteuliwa kama mgombea mwenza wa Gladys Wanga.

Odinga alisema kwamba katiba ya chama hicho inawarusu kumchagua mgombea wao baada ya kufanya mazungumzo ya kina.

Viongozi wote sasa walitakiwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha wanaibuka kidedea katika uchaguzi wa Agosti 9.