logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi wakamata mshukiwa mmoja na kunasa bastola eneo la Merti

Alipokaguliwa alipatikana na bastola ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya miraa.

image
na Davis Ojiambo

Habari06 May 2022 - 12:54

Muhtasari


  • • Sharamo alikuwa ameabiri basi kulekea Moyale na alikuwa na miraa aliyokuwa amefunga ndani ya jani la mgomba.
  • • Polisi walipomkagua zaidi walipata risasi mbili zaidi.
  • • Uchunguzi umeanzishwa kubaini kama bastola hiyo imetumika katika visa vya uhalifu.
Bastola na risasi zilizonaswa na polisi kwenye barabara kuu ya Isiolo-Moyale.

Kikosi cha pamoja cha maafisa kutoka vitengo mbalimbali vya polisi wamemtia mbaroni mshukiwa mmoja na kunasa bastola kwenye barabara kuu ya Isiolo-Moyale.

Kulingana na idara ya DCI Abdulahi Hussein Sharamo alikamatwa mapema siku ya Ijumaa katika kizuizi cha polisi na bastola aina ya P29 kupatikana kwake.

Katika ujumbe wake kwenye Twitter DCI ilisema kwamba polisi walikuwa tu wanafanya msako wa kushtukiza kwa abiria wanaotumia barabara hiyo.

Sharamo alikuwa ameabiri basi kulekea Moyale na alikuwa na miraa aliyokuwa amefunga ndani ya jani la mgomba.

Alipokaguliwa alipatikana na bastola ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya miraa.

Polisi walipomkagua zaidi walipata risasi mbili zaidi. Mshukiwa ametiwa mbaroni na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Archer katika kaunti ya Samburu.

Taarifa ya DCI ilisema kwamba atafikishwa mahakamani kwa kosa la kuwa na bunduki bila leseni. Uchunguzi pia umeanzishwa kubaini kama bastola hiyo imetumika katika visa vya uhalifu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved