logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mgomo wa wahudumu wa matatu wasababisha msongamano mkubwa Waiyaki Way

Wahudumu wanapinga kuondolewa kwa kituo cha mabasi kilichokuwa karibu na mzunguko wa Westlands.

image
na Samuel Maina

Habari19 May 2022 - 06:42

Muhtasari


  • •Wafanyakazi wa matatu walikuwa wakipinga kuondolewa kwa kituo cha mabasi kilichokuwa karibu na mzunguko wa Westlands ambao ulifungwa hivi majuzi.
  • •Polisi waliokuwa kwenye barabara hiyo waliwaelekeza madereva kutumia njia mbadala kufika walipokuwa wanaenda.
Msongamano mkubwa wa magari washuhudiwa Waiyaki Way mnamo Mei 19, 2022

Msongamano mkubwa wa magari ulishuhudiwa kwenye barabara ya Waiyaki Way jijini Nairobi Alhamisi asubuhi baada ya sehemu ya wahudumu wa matatu kugoma na kufunga barabara.

Polisi na maafisa wa GSU walilazimika kutumia vitoa machozi kutawanya umati wa watu waliokuwa wamekusanyika katika mzunguko wa Westlands.

Wafanyakazi wa matatu walikuwa wakipinga kuondolewa kwa kituo cha mabasi kilichokuwa karibu na mzunguko wa Westlands ambao ulifungwa hivi majuzi.

Wahudumu wa magari walifanya maandamano, wakizuia pande zote mbili za barabara, na kutatiza mwendo wa magari.

Baadhi ya watu wanaotumia barabara ya Waiyaki ambao walipatikana na msongamano huo walilazimika kutembea umbali mrefu  kufuatia usumbufu huo.

Polisi waliokuwa kwenye barabara hiyo waliwaelekeza madereva kutumia njia mbadala kufika walipokuwa wanaenda.

Waendesha magari waliopatikana na msongamano huo walionekana kughadhabishwa na tukio hilo ambalo lilichelewesha safari zao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved