logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tanzia: Uhuru amuomboleza mjukuu wa aliyekuwa shujaa wa ukombozi Dedan Kimathi

Uhuru alisema Teddy atakumbukwa kwa upendo na kuwa kielelezo bora kwa vijana.

image
na Davis Ojiambo

Habari19 May 2022 - 14:04

Muhtasari


  • • Rais Kenyatta alimtaja marehemu Teddy Mukaria kuwa mtu wa mwelekeo, manufaa na matumaini makubwa.

Rais Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa rambirambi kwa Mama Mukami Kimathi na familia yote ya shujaa wa ukombozi Dedan Kimathi kufuatia kifo cha mjuu wao Teddy Mukaria Githinji.

Katika ujumbe wake wa faraja na himizo siku ya Alhamisi, Rais Kenyatta alimtaja marehemu Teddy Mukaria kuwa mtu wa mwelekeo, manufaa na matumaini makubwa.

“Familia yangu na mimi mwenyewe tunahuzunishwa na msiba huo mkubwa. Akiwa na umri wa miaka 25 pekee, Teddy alikuwa mtu barubaru, mwenye mwelekeo, manufaa na matumaini makubwa. Aidha alikuwa kijana mwenye talanta aliyependa uhifadhi wa mazingira.

“Kifo chake ni pigo kubwa kwa familia ya Dedan Kimathi na namuomba Mwenyezi Mungu kuipa faraja wakati huu mgumu," kasema Rais.

Kiongozi wa Taifa alisema marehemu Teddy atakumbukwa kwa upendo kwa kuwa kielelezo bora zaidi kwa vijana.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved