logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Raila afanya mashauriano na Museveni ikulu ya Entebbe

• Raila ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa wagombeaji wa wanaoangaliwa katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, alimtembelea Rais Museveni Alhamisi jioni. • Odinga anatarajiwa kukabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa Naibu Rais William Ruto anaewania kupitia tiketi ya muungano wa Kenya Kwanza.

image
na Radio Jambo

Makala20 May 2022 - 11:42

Muhtasari


• Raila ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa wagombeaji wa wanaoangaliwa katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, alimtembelea Rais Museveni Alhamisi jioni.

• Odinga anatarajiwa kukabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa Naibu Rais William Ruto anaewania kupitia tiketi ya muungano wa Kenya Kwanza.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni akishauriana na kiongozi wa Azimio Raila Odinga

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anasema mazungumzo na mgombea urais wa Kenya, Raila Odinga yaliyofanyika Ikulu ya Entebbe yaligusia masuala yanayohusu nchi hizo mbili jirani.

Bw Odinga, ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa wagombeaji wa wanaoangaliwa katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, alimtembelea Rais Museveni jana jioni.

Katika ujumbe wake wa Twitter kuhusu mkutano huo, Bw Odinga alisema wamejadili historia ya pamoja ya nchi zao inayolenga kuimarisha uhusiano wa siku zijazo.

Siku mbili zilizopita, Odinga alikuwa Sudan Kusini ambako alikutana na Rais Salva Kiir na kuzindua Daraja la Uhuru la kilomita 3.6 linalotarajiwa kurahisisha usafirishaji wa bidhaa katika Mto Nile.

Orodha ya wagombea urais 55 wameidhinishwa kugombea katika uchaguzi wa Kenya.

Odinga anatarajiwa kukabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa Naibu Rais William Ruto anaewania kupitia tiketi ya muungano wa Kenya Kwanza.

Uchaguzi wa Kenya ni muhimu katika kanda hiyo kwa sababu ndio mahali pa kuingizia bidhaa kutoka nchi zisizo na bandari kama vile Uganda, Sudan Kusini na Kongo DR.

Eneo hilo litakuwa na wasiwasi kutokana na uchaguzi uliokumbwa na ghasia wa mwaka 2007 ambao uliathiri uchumi wao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved