Jina la kampuni ya Kijapani lilivyozua taharuki mitandaoni

Muhtasari

• Neno hilo kwa kawaida si la staha kutamkwa hadharani kwa maana ya Kiswahili.

Image: Getty Images

Wakenya wengi mtandaoni na wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kwingineko wanaelezea mshtuko wao na wakizua mjadala kuhusu jina la kampuni mpya ya Naomi Osaka iliyozinduliwa.

Jina la kampuni ya vyombo vya habari lenye maana ''hana sehemu za siri'' kwa kiswahili ambayo Osaka amezindua kwa ushirikiano na bingwa mara nne wa NBA LeBron James - imezua taharuki na imekuwa ikivuma kwenye mtandao waTwitter.

Neno hilo kwa kawaida si la staha kutamkwa hadharani kwa maana ya Kiswahili.

Vyombo kadha vya habari nchini Kenya, vimeandika kuhusu mada hiyo vikihoji kwa nini Wakenya wamekuwa wakijadili kwa kiasi kikubwa mtandaoni jina la kampuni hiyo.

Kampuni ya utayarishaji imesema itakuwa ikitengeneza hadithi ambazo "ni maalum kitamaduni lakini za ulimwengu kwa watazamaji wote" na zinalenga "kushughulikia masuala muhimu ya jamii".