Kijana mmoja kutoka nchini Afrika Kusini alifariki baada ya kukunywa pombe aina Jagarmeister kwa chini ya dakika mbili kwenye mashindano ya unywaji pombe.
Mwendazake alionekana kwenye video iliyosambaa kwenye mitandao akibugia kinywaji hicho huku watu wakimshangalia.
Tukio hili ilifanyika katika mojawapo ya maeneo ya kuuza pombe za kienyeji huko Waterval Limpopo, Afrika Kusini.
Pesa takriban Randi mia mbili ambazo ni sawa na Ksh.1,400 za Kenya zilitengwa kama zawadi kwa yule ambaye angeshinda katika shindano hilo.
''Mshindi ambaye anaweza kukunywa haya pombe kwa kutumia muda mfupi mno atapata zawadi ya Pesa R 200'' moja ya vyombo vya habari ilidaiwa kuwa Bw. Majopelo alisema.
Kijana huyo mwenye umri kati ya (25-30) alikimbizwa hospitalini na baada ya muda mfupi akatangazwa kuwa amefariki.
"Ni kitu cha kushangaza sana... kwani... hii sio kitu cha kuchekesha hata kidogo ... ulikuwa mchezo ambao haukuwa sawa kutoka pande zote kwa mwaadhiriwa pamoja na yule ambaye aliandaa ile mashindano," Mteja mmoja alitoa maoni yake.
Kinywaji hicho chenye kiwango cha 750ml ya Kijerumani kilichotengenezwa kwa mimea na viungo tofauti kina pombe kwa kiwango cha asilimia 35.
Polisi wa Limpopo sasa wameanza uchunguzi kuhusu kile ambacho kinadaiwa uenda kilisababisha kifo cha huyo Kijana.