logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kondakta ampiga mwenzake kwa mawe hadi kufa katika mzozo kuhusu abiria Nairobi

Polisi wanasema mshukiwa ambaye anajulikana kama "Johny" alitoroka na bado hajapatikana.

image
na Samuel Maina

Habari25 July 2022 - 11:03

Muhtasari


  • •Stephen Mkubwa alifariki katika hospitali moja ya mtaa wa mabanda wa Mathare baada ya kupigwa kwa jiwe na kondakta mwenzake.
  • •Polisi walisema mzozo uliosababisha kifo ulitokea katika kituo cha mabasi ambapo makondakta walikuwa wakichukua abiria kuwapeleka jijini Nairobi.

Polisi wanamsaka manamba aliyempiga na kumuua mwenzake kwa jiwe walipokuwa wakizozania abiria katika eneo la Mlango Kubwa jijini Nairobi.

Stephen Mkubwa, 32, alifariki katika hospitali moja ya mtaa wa mabanda wa Mathare baada ya kupigwa kwa jiwe na kondakta asiyejulikana.

Polisi wanasema mshambuliaji ambaye anajulikana katika eneo hilo kama "Johny" alitoroka na bado hajapatikana.

Mkuu wa polisi wa Nairobi James Mugera alisema mzozo uliosababisha kifo ulitokea katika kituo cha mabasi ambapo makondakta walikuwa wakichukua abiria kuwapeleka jijini Nairobi.

Aliongeza kuwa walimhoji dereva wa basi ambalo mshukiwa alifanya kazi na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti ambapo uchunguzi umepangwa kama sehemu ya uchunguzi wa kifo chake.

Kwingineko, mfanyakazi wa ujenzi alikufa baada ya kuanguka kutoka orofa ya nne ya jengo alilokuwa akifanyia kazi.

Mwili wa Hilary Nduzo ulipatikana kwenye ghorofa ya chini ya jengo hilo Jumapili asubuhi, muda mrefu baada ya tukio hilo kutokea.

Walioshuhudia walisema damu ilikuwa ikitoka puani na mdomoni wa marehemu na alikuwa amevunjika mkono.

Polisi wanashuku kuwa aliangukia kichwa chake na mkono wa kushoto. Mwili uligunduliwa Jumapili asubuhi, siku moja baada ya tukio hilo kutokea.

Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Polisi wanasema wamekuwa wakirekodi visa vilivyoongezeka vya vifo katika maeneo ya ujenzi huku kukiwa na wito wa ulinzi wa wafanyikazi katika maeneo kama hayo.

Maafisa wa Mamlaka ya Kitaifa ya Ujenzi wametoa wito kwa wanakandarasi kuweka mikakati ya kukabiliana na tishio hilo.

Wakati huo huo, mshukiwa wa jambazi alipigwa risasi na kufa Jumapili usiku katika jaribio la wizi lililoshindikana katika kituo cha mafuta cha Syokimau, Machakos.

Mwathiriwa anasemekana kuwa miongoni mwa genge la wanaume wanne ambao walimteka mhudumu katika kituo cha mafuta wakidai pesa wakati polisi walipoarifiwa.

Polisi waliokuwa wakishika doria walikimbilia hapo na kulikimbiza genge hilo kabla ya kumpiga risasi na kumuua mmoja wa washukiwa huku wengine wakitoroka kwa pikipiki.

Polisi wanasema walipata bastola kutoka kwa mshukiwa aliyeuawa kabla ya kuupeleka mwili wake kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Na moto uliteketeza madarasa 14 ya shule ya msingi huko Kawangware, Nairobi na kuwaacha wengi bila makazi.

Moto huo ulizuka katika shule ya msingi ya Lindi Friends kutoka katika moja ya majengo yaliyoathirika kabla ya kusambaa kwa maeneo mengine.

Kuna karibu wanafunzi 300 ambao wanasoma katika shule hiyo na walifika shuleni leo na kukuta madarasa yao yameteketea. Polisi wanasema wanachunguza tukio hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved