logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilizungumza na Wajackoyah mara ya mwisho Agosti 3- Justina Wamae

Wamae alidai Wajackoyah alimblock na hawajawasiliana naye isipokuwa wakati walipokutana Bomas ambapo walisalimiana.

image
na Samuel Maina

Habari24 August 2022 - 08:34

Muhtasari


  • •Wamae sasa anadai alizungumza mara ya mwisho na bosi wake kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
  • •Wamae alidai chama chake hakina mpangilio na uhamasishaji wao wa maajenti kwa uchaguzi ulikuwa duni.
Mgombea Urais wa Roots Party George Wajackoyah na mgombea mwenza wake Justina Wamae.

Mgombea mwenza wa urais wa Chama cha Roots, Justina Wamae ameendelea kufunguka kuhusu uhusiano wake na kiongozi wa chama George Wajackoyah.

Wamae sasa anadai alizungumza mara ya mwisho na bosi wake kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

"Mara ya mwisho nilifanya mazungumzo na kiongozi wa chama changu ilikuwa Agosti 3, hiyo ilikuwa kabla ya uchaguzi," alisema wakati wa mahojiano na televisheni moja siku ya Jumanne.

Wamae alidai baada ya hapo, Wajackoyah alimblock na hawajawasiliana naye isipokuwa wakati walipokutana Bomas of Kenya wakati wa kujumlisha kura - na walisalimiana tu.

"Hatujazungumza naye kuhusu masuala ya uchaguzi na chama chetu ana kwa ana," Wamae alifichua.

Uhusiano kati ya wanasiasa hao wawili umegonga mwamba na kusababisha wito wa kinidhamu kwa Wamae.

Mgogoro unahusu matamshi ya Wamae hadharani ambayo hayawiani na msimamo wa chama chao.

Miongoni mwao ni matamshi kuwa Wajackoyah aliidhinisha mgombea urais wa Azimio Raila Odinga kabla ya uchaguzi, nafasi ambayo kiongozi wa chama chake alipuuzilia mbali kama uongo.

Katika barua ya mkurugenzi wa masuala ya sheria Washika Wachira, chama hicho kilimkashifu Wamae kwa kukiuka miundo ya chama na kuchafua sifa ya chama.

Wamae, hata hivyo, alipuuzilia mbali wito huo akisema hawezi kujibu mambo madogo.

Wakati wa mahojiano Jumanne, Wamae alidai chama chake hakina mpangilio na uhamasishaji wao wa maajenti kwa uchaguzi ulikuwa duni.

"Sababu iliyonifanya kusema kuwa chama chetu hakijajiandaa ni ukweli kwamba yeye (Wajackoyah) hakutaka kuzungumza nami kama mshirika wake wa karibu,"

Wamae, hata hivyo, alisema kuwa licha ya changamoto hizo, hakuona ni busara kuzitangaza hadharani.

Anataka masuala yatatuliwe kwa kikao cha moja kwa moja na sio kwenye mitandao ya kijamii.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved