Gari la gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Junior lilihusika katika ajali kabla ya hafla ya kuapishwa kwake.
Ajali hiyo ilitokea katika Barabara ya Machakos-Wote karibu na Wote Town mwendo wa saa nne unusu asubuhi.
Duru za kuaminika ziliarifu kuwa watu watatu waliokuwa ndani waliweza kunusurika bila majeraha.
Mutula hakuwa miongoni mwa watu waliokuwa kwenye gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser V8 wakati ajali ilipotokea.
Kilonzo alitumia gari tofauti kufika eneo la tukio la kuapishwa.
Inasemekana gari hilo lilipoteza udhibiti kabla ya kutua kwenye mtaro.
Mengine yanafuata...