logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wizi wa mifugo lazima ukome na sio tafadhali-Rais Ruto asema

Haya yanajiri baada ya maafisa 8 wa usalama kupoteza maisha kutokana na wizi wa Ng'ombe.

image
na Radio Jambo

Burudani25 September 2022 - 18:40

Muhtasari


  • Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa alikuwa akiunga mkono wazo la Ruto na anahimiza wizi wa Ng'ombe ukome mara moja

Rais Dkt William Samoei Ruto hatimaye amekabiliana na wizi wa Ng'ombe Kaskazini Mashariki mwa Kenya. Wizi wa mifugo umekuwa mkali sana kwa muda mrefu.

Hii inapelekea jamii za wafugaji kupoteza mifugo na pia kupoteza wanafamilia wao wapendwa.

 Ruto amechukua hatua ya kuagiza mashirika ya usalama kukabiliana vilivyo na waathiriwa wa wizi wa Ng'ombe Turkana na Pokot.

Haya yanajiri baada ya maafisa 8 wa usalama kupoteza maisha kutokana na wizi wa Ng'ombe.

Ruto Baada ya kupokea ripoti ya kina kuhusu tukio la Turkana/Pokot ambalo lilisababisha maafisa 8 wa usalama/utawala kupoteza maisha, aliagiza vyombo vya usalama kushughulikia kwa uthabiti, kwa uamuzi na kwa ukamilifu na wale wanaohusika. 

" Baada ya kupokea ripoti ya kina kuhusu tukio la Turkana/pokot lililosababisha maafisa 10 wa usalama/utawala kupoteza maisha, nimeagiza mashirika ya usalama kushughulikia kwa uthabiti, madhubuti na kwa uthabiti. pamoja na wanaohusika. Cattle rustling will stop na sio tafadhali.

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa alikuwa akiunga mkono wazo la Ruto na anahimiza wizi wa Ng'ombe ukome mara moja.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved