logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Baba mkwe wa DJ Brownskin avunja kimya kuhusiana na video ya binti yake akinywa sumu

Mwangi alisema Brownskin angempeleka mkewe hospitalini badala ya kumwacha afe.

image
na

Habari04 April 2023 - 11:43

Muhtasari


• Mwangi alisema kuwa hakuwa na habari ya ugomvi wao kwa kuwa walikuwa na furaha na walimtembelea mara kwa mara na wana wao wawili.

Baba Mkwe wa DJ Brownskin avunja ukimya kuhusu mkwe wake kurekodi bintiye akinywa sumu.

Baba mkwe wa DJ Brownskin ameongea baada ya ufichuzi wa hivi punde kwamba DJ Brownskin alimrekodi mkewe akinywa sumu.

Simon Mwangi ,ambaye ni babake marehemu Sharon Njeri, aliyekuwa mke wa DJ Brownskin alisema kuwa hakufahamu ugomvi wowote uliokuwa ukiendelea baina ya Brownskin na mke wake.

Alisema kuwa anachojua ni kuwa mwanawe alikunywa sumu na alipata habari ya kifo chake alipokuwa kazini. Mwangi alilalamika kuwa amekumbana na matukio haya mapya  kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kupona  kwa kumpoteza binti yake.

Mzee Mwangi aliongeza kusema ataridhika tu haki ya marehemu bintiye ikipatikana.  Alisema haikuwa vizuri kwa Brownskin kuchukua video ya mke wake akinywa sumu.

"Huwezi chukua video ya mtu ambaye mmezaa naye watoto akifa ...alikufa kwa sababu alikuwa anakupenda ilhali wewe unamchukua video akifa, hiyo ndiyo zawadi waweza kumpa?" alisema Simon.

Mwangi alisema Brownskin alikuwa na nafasi ya kumpeleka mkewe hospitalini badala ya kumwacha afe.

Sharon Njeri aliaga mwaka uliopita baada ya kunywa sumu iliyomwangamiza.

Hivi majuzi, video iliibuka mtandaoni Njeri akionekana akinywa sumu hiyo.

 Jambo hilo lilizua hisia mseto huku watu wengi wakigadhabishwa na kumnyooshea kidole  DJ Brownskin wakidai kuwa lilikuwa ni tendo la kukosa ubinadamu kwa kuchukua video hiyo badala ya kuokoa maisha yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved