logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wakenya kupata vitambulisho vya kidijitali vinavyoweza kusomeka kwa mashine

Kindiki alisema kuwa katika siku zijazo, Kenya inatafuta kuboresha mfumo wake wa sasa wa utambuzi wa alama za vidole.

image
na

Habari24 May 2023 - 11:19

Muhtasari


•Kindiki alisema kuwa katika siku zijazo, Kenya inatafuta kuboresha mfumo wake wa sasa wa utambuzi wa alama za vidole.

•Kindiki pia aliongeza kuwa Kenya itahamia kitambulisho cha kielektroniki chenye ‘chip’ inayoweza kusomeka kwa mashine na msimbo wa QR.

wakati wa Mkutano wa Vitambulisho vya Afrika huko Nairobi Mei 24, 2023.

Kila kitu kinaelekea mitamboni huku Kenya ikijiandaa kukumbatia mfumo wa utambuzi wa kibayometriki kutumia mitambo.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa Kithure Kindiki Jumatano alisema kuwa katika siku zijazo, Kenya inatafuta kuboresha mfumo wake wa sasa wa utambuzi wa alama za vidole kuwa mfumo wa kitambulisho wa kibayometriki wa moja kwa moja.

"Kwa sasa, tuna mfumo wa vitambulisho nchini Kenya ambao ni wa nusu-otomatiki. Kwenda mbele tunaangazia kuboresha mfumo wa vitambulisho kiotomatiki wa alama za vidole," alisema.

Mfumo wa kitambulisho otomatiki wa kibayometriki kulingana na waziri utaenda zaidi ya alama ya vidole, ikihusisha jicho pamoja na utambuzi wa uso.

Kindiki pia aliongeza kuwa Kenya itahamia kitambulisho cha kielektroniki chenye ‘chip’ inayoweza kusomeka kwa mashine na msimbo wa QR.

"Hii inapaswa kutupeleka kwenye mfumo wa Kitambulisho wa kidijitali ambao utaruhusu uthibitishaji wa kitambulisho kwenye wavuti," alisema.

Kindiki aliongeza kuwa baada ya muda mrefu, uthibitishaji wa kitambulisho cha mtandaoni utapitishwa hadi katika kitambulisho cha kipekee cha kimataifa ambacho serikali itawapa watoto wachanga wote nchini Kenya na kuwa kitambulisho chao pindi watakapofikisha umri wa miaka 18.

“Itakuwa namba yao ya Nemis (Mfumo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Taarifa za Elimu) wakiwa shuleni, watakapofikisha miaka 18, itakuwa ni kitambulisho, NHIF, NSSF na itakuwa namba ya cheti chako cha kifo,” alisema Februari.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved