Majambazi wanaswa kwenye CCTV wakivamia Kanisa Embakasi

Wizi kanisani huku wahalifu wakitoweka na sadaka ya kanisa

Muhtasari

•Polisi wameazisha uchunguzi  kuhusiana na wizi kwenye kanisa la Deliverance eneo la Embakasi.


majabazi kutoweka na mali ya kanisa

Majambazi walionaswa kwenye kamera za CCTV wakivamia Kanisa moja eneo la Embakasi, wanasemekana kuiba bidhaa na pesa taslimu vyenye thamani ya shilingi milioni nne. 

Maafisa wa upelelezi jijini Nairobi wanachunguza kisa cha wizi katika Kanisa la Deliverance Embakasi kilichotokea alfajiri ya Jumatatu.

Kanda za CCTV zinaonyesha majambazi wanne wakiingia katika majengo ya kanisa na kutoroka na vifaa vya thamani. 

Picha zaonyesha kuwa majambazi wanne walifika eneo hilo mwendo wa saa saba na dakika 39 usiku wakiwa wamefuniko nyuso ili kuficha utambulisho wao. Waliswa na CCTV walimfunga mlinzi kabla ya kuingia kanisani.

Baadaye walionekana wakitoka na mabegi na vitu vingine vya thamani. Mmoja wa majambazi hao alinaswa akitafuta kitu katika eneo la juu la kanisa hilo na ndipo alipoona moja ya kamera za CCTV na kumulika mwanga wake.

Tukio hilo la wizi lilidumu kwa zaidi ya saa 2. Kulingana na wachungaji wa Kanisa la Deliverance, majambazi hao walichukua Ksh.400,000 kwenye sefu ya kanisa, ala za muziki, skrini tano, kibodi mbili, kichanganya sauti, kamera mbili, laptop mbili, kompyuta, na amplifaya mbili zinazokadiriwa kuwa za Ksh. milioni 4.

Wizi huo uliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Embakasi huku maafisa wa upelelezi wakianza uchunguzi.