Kundi la vijana waliokwenda Malaysia kutafuta kazi wanalilia haki baada ya kutelekezwa na mwajiri wao ambaye akiwafuta kazi bila malipo.
Watano hao; Charles Macharia, Geoffrey Maina, David Kevin Ochola, Dickson Otieno na Sospeter Ngahu wanasema wamekuwa wakilala kwenye ngazi za ghala lililotelekezwa huko Johor Bahru, mwendo wa saa tano kwa gari kutoka mji mkuu Kuala Lumpur.
Kwenyemahojiano na Citizen , mabwana hao walisimulia jinsi walivyopelekwa Malaysia kupitia wakala wa Kenya aliyetambulika kama David mnamo Aprili 2023, kwa ahadi ya nafasi bora za kazi.
Walipoguswa, walikabidhiwa kwa wakala wa Malaysia aliyejulikana kama Annand, ambaye aliwapeleka kwa kampuni ya usafirishaji huko Johor Bahru.
Wanasema zadi ya miezi miwili hawakupokea malipo yao, na walipouliza wakaambiwa kuwa wamelipwa kupitia ajenti wao Annand.
Ngahu alisimulia kwa simu kwa njia ya video akisema;
"Tumekuwa tukilala kwenye katoni hizi kwa kuwa hatuna chochote. Tumekwama hapa na hata kampuni ilikatisha ajira na kutupa notisi ya kuondoka kwenye ghala hili ifikapo Septemba 1. Lakini hatuna pa kwenda,"
Juhudi zao za kuitisha pesa kutoka kwa ajenti huyo ziligonga mwamba baada ya ajenti huyo kuonyesha ujeuri
Ngahu aliongeza kueleza masaibu yao akisema kuwa.
"Tunahisi tuliuzwa hapa kama watumwa kwa sababu Annand alisema ametununua na ndiyo maana hatulipwi. Huu ni utumwa wa siku hizi,"
Watano hao wamefanya kila juhudi kupata usaidizi unaohitajika kurejea nchini ila zimegonga mwamba.
Kufikia sasa, wamejilimbikizia faini ambazo wanapaswa kulipa kwa serikali ya Malaysia kabla ya kuondoka. Hizi ni faini kwa kukaa zaidi na kila mmoja wao anahitaji Ksh35,000 kama faini.
Safari ya ndege ya kurejea Nairobi kutoka Kuala Lumpur itagharimu kila mmoja wao Ksh70,000. hii inamaanisha kuwa shilingi elfu 105,000 kila mmoja wao ataweza kurudi Kenya na kuanza upya.
"Familia zetu hazina aina hiyo ya pesa, ndio maana tumekwama hapa. Kila siku wanalimbikiza madeni na hiyo inamaanisha hata tukirudi nyumbani tutaanza kutoka sifuri," Ngahu aliongeza.
Juhudi za kupata usaidizi kutoka kwa ubalozi wa Kenya nchini Malaysia hazijazaa matunda pia. Ubalozi huo unasema unaweza kuwasaidia iwapo tu watakusanya pesa za faini na tiketi za ndege za kwenda Nairobi.
Watano hao wameitaka serikali ya Kenya kuingilia kati ili kuwasaidia kurejea nyumbani kwa familia zao.
"Tunachoomba ni msaada wa kurejea nyumbani. Tulikuja hapa kujisaidia na familia zetu lakini tukagundua tulidanganywa. Mawakala wa Kenya na Malaysia wanajua wanachofanya. Tafadhali tusaidie kurudi nyumbani," .