Athari za uraibu wa mtu kujimalizia hisia za mapenzi

Washauri wa maswala ya ndoa wanaonya kuwa mazoea ya kujichua pia mara nyingi huharibu uhusiano kati ya wapenzi.

Muhtasari

•Wengi wa wanarika hupatwa na msongo wa mawazo kutokana na athari za kujichua

punyeto yaharibu ndoa nyingi za vijana
punyeto yaharibu ndoa nyingi za vijana
Image: maktaba

Uraibu wa wanawake au wanaume kujimalizia hisia zao za kimapenzi ni tatizo ambalo linazidi kukithiri katika jamii na tushia ndoa nyingi miongoni mwa wanajamii.

Hiki ni kitendo cha mtu kutomasa sehemu zake za siri mwenyewe ili kujisisimua kimapenzi.

Kitendo hiki kulingana na wataalam ni cha kawaida lakini kikifanywa muda mrefu huathiri uwezo wa muhusika kutekeleza majukumu yake ya chumbani hasa kwa wanaume ikiwa ameoa. 

Kupotea kwa nguvu za kiume: kuligana na washauri wa maswala ya ndoa  ni wazi kuwa wengi wa vijana ambao ni waraibu wa kitendo hiki huchagia sana mtu kupoteza uwezo wa mwanamume kumridhisha mpenziwe kwa sababu kutumia mikono yao kujichua huathiri mishipa ya fahamu inayoenda kwenye uume.

Utasa wa muda kwa wanaume: Mazoea haya pia hupunguza sana kiasi cha manii kinachopatikana kwenye korodani hali inayopunguza uwezo wa mwanamume kumtunga mwanamke mimba.

Jambo hili la kukosa watoto ndani ya familia husababisha hali aa swintofahamu katika ndoa na kuchangia msongo wa mawazo miongoni mwa vijana.

Washauri wa maswala ya ndoa wanaonya kuwa mazoea ya kujichua pia mara nyingi huharibu uhusiano kati ya wapenzi kwani kila mmoja hana hamu na mwenzake kwa sababu kila anapokuwa na hisia za kimwili anajitimizia hali ambayo ikiendelea kwa muda husambaratisha ndoa.

Kushidwa kufikisha mwenzako kileleni: Waraibu wengi wa kujichua  hasa wanaume hushindwa kuhimili tendo la ndoa kwa wakati ufaao na kumaliza safari mapema kabla ya ndege ya wenzao kutua uwanjani.