Mume amuua mkewe kwa kukaa kwao kwa muda mrefu - Busia

Caren Auma alizidisha muda wa kukaa nyumbani kwao

Muhtasari

•Kwa mujibu wa polisi wawili hao walizozana kuhusu masuala ya nyumbani kabla ya mshukiwa kumpiga Auma ngumi na kumuua wikendi

Mwanaume amuua mukewe Busia
Crime Scene Mwanaume amuua mukewe Busia
Image: HISANI

Mwanamume mwenye umri wa miaka 30 ambaye alimpiga mkewe hadi kufa katika kijiji kimoja kaunti ya Busia kwa kukaa kupita kiasi kwa wazazi wake amekamatwa.

Mshukiwa alikamatwa kufuatia kifo cha Caren Auma, 23, mama wa watoto wawili katika kijiji cha Igigo kitongoji cha Bulemia.

Kwa mujibu wa polisi wawili hao walizozana kuhusu masuala ya nyumbani kabla ya mshukiwa kumpiga Auma ngumi na kumuua wikendi.

Polisi waliotembelea eneo la tukio walisema walibaini kuwa marehemu alikuwa amewatembelea jamaa zake nchini Uganda na kukesha kinyume na mapenzi ya mumewe.

Hili lilimkasirisha na aliporudi, ugomvi ulizuka na kusababisha makonde ya kifo.

Polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti kabla ya kumkamata mshukiwa.

Polisi walisema mkshukiwa atawasilishwa kotini kwa mashtaka ya kuua wakati ambapo wanaendele ana uchunguzi wa kuwasaka watu watatu wanaoshukiwa kuwa waalifu katika eneo hilo.

Washukiwa hao wanadaiwa kuwa wezi ambao wananyanyasa watu wa eneo la nyalenda , Kaunti ya Kisumu ambapo mwanamume mmoja aliuawa na umati kwa madai kuwa aliiba tairi za tuk-tuk.

Abraham Omondi  mwenye umri wa miaka 26, alipigwa kwa mawe na umati hadi kufa kisha wakatoroka baada ya kuarifiwa kuwa polisi wangefika maeneo hayo

Kisa kingine sawia na hiki kilitokea huko Rodi, Homabay, ambapo Odiwuor Onyinge, 30, aliuawa na kundi la watu kwa madai ya kuwa jambazi.

Kesi za uvamizi wa makundi ya watu zimekuwa zikiongezeka katika vijiji, ambavyo vingi vinahusishwa na wizi wa mabavu na matatizo ya ndoa kwenye familia.

Polisi wamewaimiza watu kutochukua sheria mikononi mwao na kusisitiza watu wafuate mkondo wa sheria ipasavyo.