Google yaadhimisha miaka 25 tangu kuzinduliwa kwake mnamo 1998

Kwenye jukwaa lake, Google imebadilisha herufi mbili 'oo' na nambari '25' ili kusherehekea kumbukumbu yake ya miaka.

Muhtasari

• Google ina bidhaa tisa zilizo na watumiaji zaidi ya bilioni moja wanaotumia kila mwezi.

• Bidhaa hizo ni pamoja na; Tafuta na Google, Android, Chrome, Gmail, Hifadhi ya Google, Ramani za Google, Google Play Store, You Tube na Picha kwenye Google.

picha Google
picha Google

Wavuti wa utaftaji Google unaadhimisha miaka 25 tangu kuzinduliwa kwake mnamo Septemba 27, 1998.

Kwenye jukwaa lake, Google imebadilisha herufi mbili 'oo' na nambari '25' ili kusherehekea kumbukumbu yake ya miaka.

Google ilizinduliwa rasmi na wanasayansi wa kompyuta wa Marekani Larry Page na Sergey Brin

Kwa miaka mingi, imekuwa mojawapo ya kurasa za utafutaji zinazotumiwa zaidi kwenye wavuti.

Mkurugenzi Mtendaji wa sasa wa Google Alphabet Sundar Pichai alitumia akaunti yake ya X Jumatano kuwashukuru watumiaji wa Google kote ulimwenguni. "Heri ya miaka 25 ya kuzinduliwa  kwa Google.

"Asante kwa kila mtu anayetumia bidhaa zetu na kutupa changamoto ya kuendelea kuwa wabunifu na kwa WanaGoogle wote,” Pichai alisema.

Katika blogu yake, wavuti  kubwa ya utafutaji iliwashukuru watumiaji wa Google kwa kuitumia kwa miaka 25 iliyopita.

Mabilioni ya watu kutoka kote ulimwenguni hutumia Google kutafuta, kuunganisha, kufanya kazi, kucheza, na mengine mengi.

"Asante kwa kubadilika nasi kwa miaka 25 iliyopita. Hatuwezi kungoja kuona ni wapi wakati ujao unatupeleka, pamoja."

Inamilikiwa na kampuni ya kimataifa ya kiteknolojia ya Marekani Google LLC inaangazia   utangazaji wa mtandaoni, teknolojia ya injini ya utafutaji, kompyuta ya wingu, programu ya kompyuta, kompyuta ya quantum, biashara ya mtandaoni na vifaa vya kielektroniki vya watumiaji.