logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa amuua mpenzi wa kitambo Meru, kisa na maana mzozo wa TV

Polisi wachunguza kifo cha mwanamke kilichosabiswa na runinga

image
na

Habari28 September 2023 - 08:07

Muhtasari


•Mwanaume huyo alidai marehemu alikwenda nyumbani kwake akiwa na jiwe na kuanza kutoa televisheni, mashine ya kuchomelea na mashine ya kusagia ili kuziuza.

•Hili lilizua mzozo kati ya wawili ambapo vita zilizuka na  kumwacha mwanamke huyo na majeraha mabaya kichwani.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 40 alifariki baada ya vita na mpenzi wake wa zamani kuhusu runinga katika kijiji kimoja kaunti ya Meru.

Mpenzi huyo wa zamani alimpiga mwanamke huyo kichwa baada ya kudaiwa kujaribu kuingia katika nyumba yake katika kijiji cha Muringambugi, polisi walisema.

Mwanaume huyo alidai marehemu alikwenda nyumbani kwake akiwa na jiwe na kuanza kutoa televisheni, mashine ya kuchomelea na mashine ya kusagia ili kuziuza.

Hili lilizua mzozo kati ya wawili hao ambao ulimwacha mwanamke huyo na majeraha mabaya kichwani.

Mwanamume huyo baadaye aliripoti kisa hicho kabla ya polisi kufika katika nyumba hiyo ambapo walimkuta mwanamke huyo akiwa na majeraha mabaya kichwani.

Mshukiwa alizuiliwa baada ya tukio hilo. Aliwaambia polisi kwamba walikuwa wametofautiana miezi iliyopita na mwanamke huyo alihama kutoka nyumbani walokoishi naye. 

Polisi walisema viti viwili, jiwe, na kitambaa cheupe chenye madoa ya damu vilipatikana na kuwekwa kama vielelezo vya ushaindi kufuatia kifo cha mwanamke huyo.

Mwili wa mwanamke huo ulichukuliwa na polisi na kusafirishwa  hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi zaidi kufuatia kifo icho.

Polisi walisema mshukiwa anatarajiwa kortini ambapo walinuia kuomba siku zaidi ili kuwawezesha kukamilisha uchunguzi wao.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved