Huku mshukiwa mkuu wa mauaji ya halaiki katika msitu wa Shakahola, Paul Mackenzie na ,watuhumiwa wenzake 28 wakisalia rumande hadi Desemba 22, 2023 mama mmoja amesimulia masaibu waliyoyapitia mikononi mwa Mackenzie.
Mama huyo ambaye alifanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha runinga alifunguka huku akisisema kuwa mfungo ndani ya msitu wa shakahola ulianza baada kuamishwa kwa ibada kutoka kanisani hadi msituni shakahola.
"Tulipoama kanisani na kwenda msituni kulikuwa na masharti mengi cha kwanza tulijulishwa kuwa ni nyakati za mwisho na tulistahili kufunga ili kuenda kukutana na Mungu,tulijulishwa kuwa watoto ndio wangeaza mfungo huo,mimi na watoto wangu tulianza mfungo huo hadi siku ya tano wakati watoto wangu walianza kudhohofika kiafya ndipo nilikimbilia usalama wangu,"alisema mama huyo.
Mama huyo wa watoto wanne alisimulia zaidi kuwa kulikuwa na wachungaji wengine kutoka nchi za kigeni ambao walishirikiana na Paul Mackenzie kutekeleza unyama huo.
"Kule jagwani kulikuwa na wachungaji wengine walioshirikiana na Mackenzie cha kushangaza tulinyimwa kusoma bibilia,kutembeleana huku elimu na matibabu ya hospitali zikipigwa marufuku,"alisema.
Kulingana na manusura huyo kunyonyesha mtoto ilikuwa imepigwa marufuku huku sheria kali ikiwekwa kwa yeyote angekeuka sheria hiyo.
Kwenye mahojiano hayo alieleza zaidi kuwa kati ya wachungaji wakuu kwenye msitu huo wao walikuwa wanakula vyakula na vinywaji licha ya kuwa waliwaonya wafuasi wao kutojaribu kukeuka sheria ya mfungo.
"Nilipoona maisha yetu yako hatarini niliwahepesha watoto wangu ila mume wangu aliwarudisha tena msituni kwa bahati nzuri tuliokolewa huku watoto wangu wakipelekwa kwenye kituo cha watoto ila mume wangu alibakia msituni na kushikwa na maafisa wa usalama pamoja na wachungaji wengine,"alisema.