logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mzee wa kijiji ang’olewa jicho na mkewe kwa madai ya kuwa na mpango wa kando

Mwanamume huyo sasa anasema anahofia kuwa anaweza kupatwa na ugonjwa wa kupooza.

image
na Davis Ojiambo

Habari31 January 2024 - 07:40

Muhtasari


  • • Mke huyo alikuwa akimshutumu mhasiriwa kwa madia ya kuwa na mipango ya kando madai yaliyozua ugomvi.
Wagonjwa wakiwasili katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kisii Ijumaa, Desemba 23. Picha: MAGATI OBEBO

Mzee wa ukoo wa Manga katika Kaunti ya Nyamira siku ya Jumanne alilazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kisii baada ya mkewe kuripotiwa kumjeruhi kwa kumpiga na nyundo kichwani. 

Mwanamume huyo, 50, pia alipoteza jicho lake la kushoto wakati wa makabiliano hayo usiku katika kijiji cha Nyaboterere.Jicho hilo limeng'olewa baada ya upasuaji.

Madaktari walisema mishipa ya jicho iliharibiwa zaidi ya kurekebishwa na hivyo kulazimika kuondolewa.

Mke huyo alikuwa akimshutumu mhasiriwa kwa madia ya kuwa na mipango ya kando madai yaliyozua ugomvi.

"Hivi majuzi alikuwa amenishutumu kwa kuchumbiana na wanawake na kwamba nilikuwa nikipoteza mapato ya familia yetu juu yao, tuhuma ambazo ni za uwongo na za kupotosha," aliwaambia waandishi wa habari kutoka kwa kitanda chake hospitalini.

Uamuzi wa kuuza sehemu ya shamba lake na kuweka pesa kwa benki ulikuwa kuwalipia wanao karo katika chuo kikuu na vyuo ya anuai. “Hatua hii hata hivyo ilizua tuhuma zaidi kutoka kwa mke,” aliongeza.

Jamaa huyo alilsema alilazimka kuiondoa na kuleta pesa zote nyumbani kwenye sanduku.

"Inaonekana hakushawishika kwamba kwamba nilikuwa nimeweka pesa benki kwa ajili ya watoto wetu na badala yake akaanza kuzunguka akinituhumu kwa uwongo miongoni mwa watoto wangu kwamba nilikuwa nimepeleka kwa makahaba," alisema.

"Ili kuleta amani nilienda na kumletea Sh260,000 zote na kumkabidhi. Ninashuku kuwa hii ina mkono katika jaribio la kuniua," alisema akiwa hospitalini Jumanne jioni.

Mwanamume huyo sasa anasema anahofia kuwa anaweza kupatwa na ugonjwa wa kupooza kwa muda mrefu kutokana na majeraha hayo na kuomba wasamaria wema kumsaidia kupata pesa za watoto wake baada ya mke kutoroka na pesa hizo.

Polisi tayari wanamsaka mwanamke huyo.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved