logo

NOW ON AIR

Listen in Live

RIP! Aliyekuwa mtangazaji wa KTN, Michael Oyier amefariki

Kulingana na rafiki wa familia, alisema Oyier alianguka katika nyumba yake Lavington jijini Nairobi mnamo Jumatano Aprili 17.

image
na SAMUEL MAINA

Habari21 April 2024 - 05:38

Muhtasari


  • •Kulingana na rafiki wa familia, alisema Oyier alianguka katika nyumba yake Lavington jijini Nairobi mnamo Jumatano Aprili 17.

Aliyekuwa mtangazaji wa KTN News Michael Oyier amefariki.

Oyier alifariki alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi.

Kulingana na rafiki wa familia, alisema Oyier alianguka katika nyumba yake Lavington jijini Nairobi mnamo Jumatano Aprili 17.

Hii ilikuwa baada ya kulalamika kuhusu maumivu makali ya kichwa.

Madaktari hawakueleza ni nini walichobaini kuwa sababu ya maumivu ya kichwa.

Uchunguzi wa maiti umepangwa kubaini sababu ya kifo cha mtangazaji huyo.

Oyier alijitosa katika PR baada ya kuondoka KTN.

Alicheza pia kama MC katika hafla kadhaa.

Wanahabari Maina Kageni na Carol Radull walimuomboleza Oyier kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Maneno ya Maina yalisomeka, "Tumepoteza legendari. Asante kwa kila kitu Michael Oyier... mmoja wa watangazaji bora sana wa habari ambao nimewahi kuwafahamu.... mfano wa kweli wa kujitolea, nidhamu na kutia moyo!!!! wanahabari wote na familia (Peter, Paul, Olga) na marafiki Rest In Peace Michael Oyier....."

Carol kwa upande wake aliandika, "Habari mbaya zaidi kuwahi kutokea. Aliyekuwa mtangazaji wa KTN na Kiss100 News Michael Oyier alifariki alipokuwa akipokea matibabu."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved