Ibada ya ukumbusho ya Jenerali Francis Ogolla yaahirishwa

Familia ya marehemu Ogolla ilisema kuwa tarehe mpya ya ibada ya kumbukumbu itatangazwa siku zijazo.

Muhtasari

• Hafla hiyo ilikuwa imeratibiwa kufanyika Ijumaa, Aprili 26, 2024, katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex huko Langata, imeahirishwa.

Picha ya jenerali Francis Ogolla
Image: EZEKIEL AMINGA

Ibada ya ukumbusho ya aliyekuwa mkuu wa Majeshi marehemu Jenerali Francis Omondi Ogolla, iliyokuwa imeratibiwa kufanyika Ijumaa, Aprili 26, 2024, katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex huko Langata, imeahirishwa.

KDF, katika taarifa ya pamoja na familia ya marehemu Jenerali, ilisema kuwa tarehe mpya ya ibada ya kumbukumbu itatangazwa siku zijazo.

Taarifa hiyo haikueleza mara moja kwa nini hafla hiyo iliahirishwa, lakini ilitaja kuwa familia hiyo ilipata heshima kubwa kwa jinsi watu walijitokeza kwa maizishi ya Ogolla.

Ogolla alifariki kutokana na ajali ya helikopta Alhamisi wiki iliyopita. Ajali hiyo pia ilisababisha vifo vya maafisa tisa wa ngazi za juu katika jeshi.