Dadake Ogolla afichua alichotaka jeshi limfanyie mjane wake baada ya kifo

Marehemu Francis Ogolla aliacha matakwa kwamba angependa yatimizwe baada ya kifo chake

Muhtasari
  • Sasa inaibuka kuwa aliomba Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) kumpa mjane wake, Aillen Ogolla likizo ya chaguo lake.
  • Peris alisema kuwa Jenerali Ogolla  alikuwa na matakwa 3 aliyotaka yatimizwe baada ya kifo chake.
Peris Onyango
Image: Hisani

Dadake Jenerali Ogolla, Peris Onyango, alifichua ombi la ndugu yake kwa wanajeshi kwa mjane wake Aileen Kathambi Ogolla.

Marehemu Francis Ogolla aliacha matakwa kwamba angependa yatimizwe baada ya kifo chake.

Sasa inaibuka kuwa aliomba Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) kumpa mjane wake, Aillen Ogolla likizo ya chaguo lake.

Haya yalifichuliwa na dadake marehemu Peris Onyango alipokuwa akitoa heshima kwa kakake wakati wa mazishi katika kaunti ya Siaya siku ya Jumapili, Peris alisema kuwa Jenerali Ogolla  alikuwa na matakwa 3 aliyotaka yatimizwe baada ya kifo chake.

Matakwa ya kwanza aliyotaja Peris, lilikuwa kuzikwa saa 48 baada ya kufa, kauli ambayo Peris alikataa haraka kulazimisha  Jenerali kuongeza ratiba.

"Aliniambia Peris ukiwa mwanajeshi unaweza kufa wakati wowote. Kwa hivyo nikifa nataka nizikwe ndani ya saa 48. Kisha nikasema 'unamaanisha nini' kisha akasema Peris najua unaweza kuwapa matatizo kwa hiyo mimi tukikuongezea saa zaidi iwe 72," alisema.

Peris aliongeza kuwa Ogolla pia alitaja mahali ambapo angetaka kuzikwa na mwishowe, alitaka jeshi kumpeleka mkewe Aileen kwa likizo.

"Aliniambia nitakapokufa baada ya mazishi, jeshi impe mama Achieng' pesa za kwenda likizo. Kwa hivyo jeshi mna kazi ya kufanya. Mama Achieng' lazima aende likizo."

Aliendelea kuongeza kuwa Ogolla alikuwa mtoto aliyependwa sana na mama yao na tangu azaliwe ameonyesha tabia ya kupendeza hadi alipoingia KDF.

Ogolla alifariki katika ajali ya helikopta mnamo Alhamisi, Aprili 18 pamoja na maafisa wengine tisa wa kijeshi na kumfanya kuwa mkuu wa kwanza wa KDF kufariki akiwa ofisini.