Wimbo tatanishi wa Embarambamba wa kumuomboleza Jenerali Ogolla wazua hisia mseto

Aliachia wimbo huo kwenye majukwaa yake baada ya marehemu Ogolla kupoteza maisha katika ajali ya ndege.

Muhtasari

•Embarambamba aliachia wimbo huo kwenye majukwaa yake baada ya marehemu Ogolla kupoteza maisha katika ajali ya ndege.

•“Ogolla, umeacha bibi wapi? Ogolla, Ogolla. Umeacha kitanda wapi, chenye ulikuwa unalalia?. Umeacha bunduki wapi, ulikuwa unatumia?,” aliimba..

Image: HISANI

Mwimbaji mwenye utata kutoka Kisii Christopher Musioma almaarufu Embarambamba amemuomboleza marehemu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Francis Ogolla kutumia wimbo.

Mwanamuziki huyo ambaye taaluma yake imekumbwa na utata mwingi aliachia wimbo huo kwenye majukwaa yake baada ya marehemu Ogolla kupoteza maisha katika ajali ya ndege.

Katika wimbo huo, Embarambamba anasikika akiimba kuhusu jinsi ajali iliyochukua maisha ya Ogolla ilivyotokea na athari ambayo kifo chake kimesababisha.

“Kifo, kifo, aibu ya nini? Umechukua Ogolla, ameacha pesa kwa benki. Umechukua Ogolla, ameacha pesa Mpesa. Umechukua Ogolla, Ogolla *3,” Embarambamba alisikika akiimba huku akicheza densi na kujiangusha chini.

Msanii huyo aliendelea kuzungumzia jinsi marehemu jenerali atakumbukwa sana kufuatia kifo chake cha bahati mbaya mnamo Aprili 18.

“Ogolla, umeacha bibi wapi? Ogolla, Ogolla. Umeacha kitanda wapi, chenye ulikuwa unalalia?. Umeacha bunduki wapi, ulikuwa unatumia?,” aliimba..

Pia alizungumzia jinsi kifo cha Ogolla kimeiacha Kenya katika maombolezo.

Wimbo huo ambao kwa sasa umekuwa ukisambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii umezua hisia mseto kutoka kwa wanamtandao huku baadhi wakikejeli, wengine wakionekana kumuelewa mwimbaji huyo mtata huku wengine wakiona ni mzaha tu.

Haya hapa maoni kutoka kwa baadhi ya watumiaji wa Instagram;-

Annyrama: Huyu sasa achinjwe Christmas.

Dida.kas: He makes me sometimes want to disown my tribe.

Mcphilipo: This guy should be tamed, there’s time for everything.. when a family us mourning, give them time to mourn their loved ones instead of making fun of it.

Ridi_ngitighore: Huyu apelekwe mental hospital.

King_manasseh_: Huyu msee hatuwezi mpeana ata Tz wakae na yeye kidogo tupumue?

Jim_carter79: Who bewitched this guy?

Haya yanajiri huku marehemu Ogolla akitarajiwa kuzikwa leo Jumapili, Aprili 21 nyumbani kwake Ng’iya huko Alego Usonga kaunti ya Siaya.

Kulingana na familia yake, ilikuwa ni matakwa yake azikwe ndani ya saa 72 baada ya kifo chake.