Afisa wa polisi auawa na gari lililokuwa kwa kasi Ruiru

Mwenzake alikuwa na aliponea kwani alisita kuvuka baada ya kuona gari hilo likienda kwa kasi mno.

Muhtasari

• Mwathiriwa alikuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Ruiru na alikuwa akishika doria ajali hiyo ilipotokea.

• Waliyoshuhudia walisema kuwa marehemu alipata majeraha ya kichwa na kuvunjika mguu wa kushoto.

• Polisi walisema msako wa kumtafuta dereva aliyehusika na tukio hilo unaendelea.

Ajali
Ajali
Image: HISANI

Afisa wa polisi aliuawa Jumatatu usiku katika ajali kwenye barabara ya Kiambu-Ruiru, kaunti ya Kiambu.

Afisa huyo alikuwa na mwenzake walipokuwa wakivuka barabara wakati aligongwa na gari lililokuwa likiendeshwa kwa kasi.

Gari hilo halikusimama baada ya tukio hilo la saa nne usiku, polisi walisema.

Mwathiriwa alikuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Ruiru na alikuwa akishika doria ajali hiyo ilipotokea.

Mwenzake alikuwa na aliponea kwani alisita kuvuka baada ya kuona gari hilo likienda kwa kasi mno.

Waliyoshuhudia walisema kuwa marehemu alipata majeraha ya kichwa na kuvunjika mguu wa kushoto.

Alitangazwa kufariki alipofika katika hospitali ya Plainsview mtaani Ruiru.

Polisi walisema msako wa kumtafuta dereva aliyehusika na tukio hilo unaendelea.

Mwili huo ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi wa maiti.