Mvulana wa miaka 18 auawa kwa kudungwa kisu, Tana River

Muhammad Mohammed Adhen aliuawa kwa kudungwa kisu na mtu anayefahamika sana alipokuwa akichunga ngamia.

Muhtasari

• Msako wa kumtafuta mshukiwa unaendelea, polisi walisema kuwa bado hawajajua chanzo cha mauaji hayo.

Crime scene
Crime scene
Image: HISANI

Polisi wanachunguza kisa ambapo mfugaji mmoja mwenye umri wa miaka 18 alidungwa kisu na kuuawa katika mabishano katika eneo la Bangale, Kaunti ya Tana River.

Muhammad Mohammed Adhen aliuawa kwa kudungwa kisu na mtu anayefahamika sana alipokuwa akichunga ngamia katika eneo hilo.

Ndugu yake na wachungaji wengine walibeba mwili huo hadi kituo cha polisi cha eneo hilo na kutoa ripoti ya tukio hilo siku ya Jumapili.

Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwingi Level Four ukisubiri uchunguzi wa maiti.

Msako wa kumtafuta mshukiwa unaendelea, polisi walisema kuwa bado hawajajua chanzo cha mauaji hayo.

Kwingineko huko Laare, Kaunti ya Meru, mwili wa Andrew Mithika, 38 ulipatikana nyumbani kwake baada ya kushukiwa kuuawa.

Polisi walisema kuwa marehemu alikuwa na jeraha kwenye mguu wake wa kushoto.

Kulingana na polisi, ilidaiwa kuwa marehemu aliuawa na watu wawili wanaojulikana ambao walikuwa wamejificha. Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali Kuu ya Maua ukisubiri uchunguzi.

Hakuna aliyekamatwa kufikia sasa, polisi walisema Jumanne.

IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO.