logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi wapiga marufuku maandamano katikati mwa Nairobi

Idara ilielezea ukosefu wa uongozi kuwa imefanya kuwa vigumu kufanyika kwa maandamano ya amani katika siku zilizopita.

image
na Samuel Maina

Habari18 July 2024 - 04:06

Muhtasari


  • •NPS imepiga marufuku maandamano katika mwa mji wa Nairobi na viunga vyake na kutoa hakikisho la usalama katika eneo hilo.
  • •Idara ilielezea ukosefu wa uongozi kuwa imefanya kuwa vigumu kufanyika kwa maandamano ya amani katika siku zilizopita.

Idara ya Huduma ya Polisi nchini Kenya imepiga marufuku maandamano katika mwa mji wa Nairobi na viunga vyake na kutoa hakikisho la usalama katika eneo hilo.

Katika taarifa yake iliyotolea Julai, 17, 2024, polisi wamekumbusha umma jukumu muhimu la idara hiyo katika usalama wa nchi kulingana na katiba.

Hayo yamejiri huku Kenya ikiendelea kushuhudia maandamano ambayo yalianza tangu mwezi Juni, kupinga Mswada wa Fedha 2024.

‘’Nchi yetu imekuwa ikishuhudia hasara kubwa, watu wamejeruhiwa, kupoteza maisha, mali na biashara zimeharibiwa,’’ taarifa ya Idara ya Huduma ya Polisi ilisema.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa imepokea taarifa kwamba baadhi ya makundi ya kihalifu yanapanga kutumia vibaya maandamano ya siku ya Alhamisi, Julai 18, 2024 kutekeleza mashambulizi na uhalifu.

Idara hiyo ilielezea ukosefu wa uongozi kuwa imefanya kuwa vigumu kufanyika kwa maandamano ya amani katika siku zilizopita.

"Kukosekana kwa uongozi katika maandamano yaliyopita kumefanya kuwa vigumu kuhakikisha itifaki za usalama zinafuatwa. Kwa sababu hiyo, hakuna maandamano yataruhusiwa katika eneo la kibiashara katikati ya mji wa Nairobi na viunga vyake kwenda mbele kuhakikisha usalama wa raia," polisi ilisema.

Raia waliombwa kuwa makini katika maeneo yenye watu wengi, kushirikiana na polisi na kutoa taarifa zozote ambazo zinaweza kusaidia kubaini uhalifu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved