Rais William Ruto amemteua waziri mteule wa Ulinzi Aden Duale katika Wizara ya Mazingira.
Wiki iliyopita, Rais alimteua Duale katika Wizara ya Ulinzi.
Wizara ya Ulinzi sasa itaongozwa na Soipan Tuya baada ya kuhakikiwa na Bunge.
Rais Ruto aliwasilisha mabadiliko hayo kupitia kwa Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang'ula.
Katika taarifa yake kupitia akaunti yake ya X, Duale alimshukuru Rais kwa kumkabidhi tena kwa hati ya mazingira.
Mteuliwa wa Waziri wa Mazingira alisema kuwa anatazamia kuhudumu katika jukumu lake jipya.
“Ninamshukuru Rais William Ruto kwa kunikabidhi kutoka Wizara ya Ulinzi hadi Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu,” akasema.
"Ninatazamia kuhudumu katika jalada langu jipya na kuhakikisha lengo ni usimamizi endelevu wa mazingira, kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kukuza juhudi za upandaji miti na uhifadhi."
Akinukuu Quran Duale amesema: "Hakika mkachukia kitu ambacho ni kheri kwenu na mkapenda kitu ambacho ni kibaya kwenu. Mwenyezi Mungu anajua, lakini nyinyi hamjui." - Quran 2:216"
Majina hayo yamepelekwa kwenye Kamati ya Uteuzi, ambayo inatarajiwa kuhakiki na kuwasilisha ripoti ya walioteuliwa ndani ya siku 28.
Siku ya Ijumaa, Rais aliteua Mawaziri 10 na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye Baraza lake la Mawaziri.