Idara ya utabiri wa hali ya hewa Kenya yatabiri kuwa mvua kubwa itashuudiwa katika maeneo tofauti tofauti humu nchini.
Idara hiyo ilisema kuwa mvua hiyo ambayo ilianza tarehe 5 Novemba itashuhudiwa hadi tarehe Novemba 7 katika maeneo mbali mbali kote nchini.
Aidha idara hiyo ilitowa ilani kwa wakaazi wa sehemu ambazo ni tambarare na huenda zikapokea maji mengi yaliyotuama, hivyo kusababisha mafuriko.
Baadhi ya maeneo ambayo yanatarajiwa kupokea mvua ni pamoja na jiji kuu la Kenya Nairobi, Magharibi mwa Kenya, maeneo ya ziwa Viktoria ,Ukanda wa bonde la ufa, Pwani pamoja na eneo la mlima Kenya.
Aidha, idara hiyo ilisema kuwa mvua hiyo itaambatana na upepo mkali katika maeneo mengine na kuwaomba wakaazi wa maeneo husika kuwa makini na kuchukua hatua ya hali ya usalama endapo hali kama hiyo itaashuhudiwa ndiposa kukwepa adhari za mvua hii.
Kwingineko pia idara hiyo imesema hali ya jua na kunyauka kutashuhudiwa kuanzia tarehe Novemba 8 na kwaivyo kuwahimiza Wakenya kuwa ange kwa utabiri zaidi wa hali ya anga sana sana maeneo ambayo hupokea mawimbi ya mda kwa mda.
Utabiri huu wa idara hii unakuja wakati ambapo maeneo mengi Kenya yamekuwa yakishuhudia jua na hali ya joto kwa kipindi takriban miezi mbili.