Idara ya utabiri wa haliya anga ya Kenya imetahadharisha
kuhusu mvua nyingi inayotarajiwa kunyesha kati ya Alhamisi Novemba 14 na Ijumma
Novemba 15 katika baadhi ya maeneo nchini.
Kupitia ujumbe kwa vyombo vya habari idara hiyo
imetahadharisha kuwa mvua ya Zaidi ya milimita 20 chini ya masaa 24 huenda
ikanyesha kwenye baadhi ya sehemu ikiwemo maeneo ya kati ya bonde la ufa, nyanda
za chini za kusini mashariki na maeneo ya kati mwa taifa ikiwemo Nairobi.
Idara hiyo imewataka Wakenya katika sehemu ambazo zitaathirika
kuchukua tahadhari ya mapema kwani majihuenda yakawa mengi na kusababisha
mafuriko.
Maeneo ya Tharaka Nithi, Nyeri, Kimbu, Meru, Embu, Kirinyaga,
Bomet, Kericho, Nakuru, Isiolo, Nyandarua, Laikipia, Machakos, Kitui, Narok
,Kajiado na Murang’a zinatarajiwa kuathirika na mvua hiyo ya siku mbili.
Vile vile, idara hiyo imesema kuwa mvua hiyo inatarajiwa
kuongezeka hata zaidi siku ya Ijumaa katika sehemu za nyanda za chini za kusini
mashariki mwa nchi,maeneo ya kati ya nchi ikiwemo Nairobi kufikia viwango vya
milimita.
Kwenye tahadhari ya idara ya hali anga, Wakenya wameshauriwa
kutoendesha gari ama kutembea kwenye sehemu zilizofunikwa na maji. Ushauri ya
kutojikinga mvua chini ya miti umetolewa ili kueouka visa vya kupigwa na radi.
Vile vile, wakaazi wa maeneo ambayo yanajulikana kushuhudia
maporomoko ya ardhi haswa kwenye miteremko ya Aberdare na Mlima Kenya wametakiwa
kuwa waangalifu.