Maafisa wa polisi kutoka kitengo cha Operation Support Unit cha DCI, wanawazuilia washukiwa wawili wa ulanguzi wa dawa za kulevywa waliokamatwa katika eneo la Ruiru.
Washukiwa hao waliokuwa katika kituo kituo kimoja cha petrol eneo hilo , walikamatwa na gramu 180 ya kokeni pamoja na misokoto kadhaa ya bangi inayodaiwa ilikuwa inangoja mnunuzi.
Kulingana na taarifa ya DCI, wawili hao wamekuwa wakitafutwa na polisi kwa kuhusika na ulanguzi wa mihadarati jijini Nairobi na sehemu kadhaa za kaunti ya Kiambu kwa muda mrefu na baada ya mawindo ya saa kadhaa, polisi walifanikiwa kuwakamata wawili hao hatimaye.
Katika msako wa polisi kwenye gari lililokuwa limeegeshwa na washukiwa hao, vidonge tisa vya kokeni vyenye thamani ya shilingi 504,000 zilipatikana kwenye gari lao pamoja na misokoto kadhaa ya bangi. Taarifa ya polisi imebaini kuwa washukiwa hao walikuwa wanauza gramu moja ya kokeni kwa shilingi 2,800.
Washukiwa hao wanazuiliwa katika kituokimoja cha polisi
jijini Nairobi wakisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya ulanguzi wa
mihadarati. Aidha polisi wanawatafuta washukiwa wengine ambao wametambuliwa
kuhusika na ulanguzi wa mihadarati.