Maafisa wa kupambana na ulanguzi wa dawa za kulevya wamemkamata mshukiwa anayedaiwa kuwa alikuwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzani wa kilogramu 2 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mnamo Alhamisi Disemba 12.
Kwa mujibu wa idara ya upepelezi wa makosa ya jinai DCI, mshukiwa huyo alikamatwa wakati wa upekuzi wa mizigo aliyokuwa nayo ambapo mashine ya kupekua mizigo ilionyesha uwepo wa bidhaa ya kutiliwa shaka ndani ya mizigo yake.
DCI imetambua kwamba mshukiwa huyo mwanamke mwenye umri wa miaka 27, alikuwa anasafiri kuelekea Doha – Qatar.
Mshukiwa huyo alipelekwa katika ofisi za pilisi wa kupambana na ulanguzi wa dawa za kulevywa ambapo msako kwenye mzigo wake ulifanywa na kupatikana kwamba bangi iliyopatikana ilikuwa ndani ya pakiti za unga wa ugali.
Mshukiwa huyo anazuiliwa na polisi huku akitaraji kufikishwa mahakamani kujibu madai atakayoshtakiwa nayo.
DCI imeelezea kujitolea kwake katika kupigana na ulanguzi wa mihadarati haswa uuzaji, usambazaji, usafirishaji na utumiaji wa dawa zilizipiogwa marufuku wakati huu wa msimu wa sherehe.
Siku chache zilizopita katibu mkuu wa usalama wa ndani na
utawala wa kitaifa Raymond Omollo aliwarejesha maafisa wa polisi ambao walikuwa
likizoni kazini ili kuimarisha usalama katika msimu wa sherehe za Krismasi na
mwaka mpya.