Mamlaka ya uchukuzi na usalama barabarani NTSA imeahidi kuwachukulia hatua za kisheria wamiliki wa magari ya utumishi wa umma ambayo yalionekana kwenye kanda ya video iliyorekodiwa yakiendeshwa kwa namna isiyostahili katika barabara moja.
Katika video iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, na shirika moja lisilo la kiserikali lenye malengo ya kuhamisisha madereva na makanga kuzingatia usalama barabarani mnamo Jumatatu asubuhi Disemba 23, magari mawili ya kuwabeba abiria 14 yaliyoenekana yakiendeshwa kwa mkondo wa wimbi kwenye barabara yenye kona.
Kwenye magari hayo, abiria walionekana wakiwa wametoa vichwa nje wengine wakiwa wamekalia kwenye madirisha ya magari hayo licha ya mwendo wa kasi uluokuwa unaendeshwa kwenye magari yenyewe.
NTSA imesema kwamba kitendo hicho kilichorekodiwa ni kinyume cha sheria ambacho hakukubaliki na tayari wamiliki wa magari hayo ya PSV wametakiwa kufika mbele ya mamlaka hiyo.
“Hili halikubaliki. Wamiliki wa magari hayo wameitwa. Tutachukua hatua.” NTSA ilisema kwa ujumbe wake kwenye mtandao wa X.
Hayo yakijiri, mamlaka hiyo ya NTSA imeendesha msako wa magari yasiyokubalika barabarani katika sehemu tofauti tofauti nchini ilikuimarisha usalama barabarani.
Mnamo Jumatatu, maafisa wa NTSA walifanya msako katika barabara ya Kakamega – Kisumu kwenye eneo la Iguhu ambapo takribani watu 13 walipoteza maisha baada ya trela kusafirisha mizigo kupoteza mweleko na kungoga magari mawili wa abiria.
Vile vile msako ulifanywa katika kaunti ya Nyamira maafisa
wakichunguza vidhibiti mwendo kwenye magari kwa mujibu wa agizo lililotolewa na
mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi.