logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Asilimia 60 ya Wakenya hawatasherehekea Krismasi na mwaka mpya na familia na marafiki - Utafiti

Asilimia kubwa ya Wakenya wanapanga kutumia msimu huu wa sherehe kuwa na familia zao licha ya matatizo ya kifedha.

image
na Brandon Asiema

Yanayojiri24 December 2024 - 12:40

Muhtasari


  • Wakenya wengi walisema hawana pesa za kusherehekea katika msimu huu wa sherehe za krisimasi na mwaka mpya.
  • asilimia 28 ya idadi iliyofanyiwa utafiti wataenda kanisani kwa maombi huku asilimia  27 watatumia muda wa sherehe hizo na marafiki.


Takwimu zilizotolewa na kampuni ya kufanya utafiti ya Infotrak zimeonyesha kwamba asilimia kubwa ya Wakenya watakosa kusherehekea sherehe za msimu huu wa krisimasi na mwaka mpya kutokana na hali ngumu ya kiuchumi kwa ukosefu wa pesa.

Kwenye takwimu hizo za ripoti iliyotolewa mnamo Jumanne, Disemba 24, siku moja kabla ya siku kuu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa waumini wa dini ya Kikiristo, Infotrak imesema kwamba asilimia kubwa ya Wakenya hata hivyo wamepanga kusherehekea msimu huu na familia zao licha ya ugumu wa hali ya maisha.

Infotrak imesema uchunguzi wao umeonyesha kwamba asilimia 63 ya Wakenya wanapanga kutumia msimu huu wa sherehe kuwa na familia zao licha ya matatizo ya kifedha.

Mbali na takwimu hiyo, utafiti huo uliofanywa na Infotrak umeonyesha kuwa asilimia 28 ya idadi iliyofanyiwa utafiti wataenda kanisani kwa maombi huku asilimia  27 watatumia muda wa sherehe hizo na marafiki.

Aidha asilimia 15 ya Wakenya waliohojiwa walisema watasalia manyumbani kwao huku asilimia ndogo ya 11 wakitumia wakati huo kwa likizo.

Hata hivyo ikilinganishwa na takwimu za miaka ya awali, asilimia 60 ya Wakenya  hawatasherehekea Krismasi na mwaka mpya pamoja na familia na marafiki kama ilivyokuwa katika miaka ya awali.

Haya ni kulingana na kura iliyofanywa na shirika la Infotrak inayoonyesha kuwa ni asilimia 40 pekee ya Wakenya ambao watasherehekea msimu huu wa sherehe na familia pamoja na marafiki.

Kwa mujibu wa Johnvin Wanyingo wa Infotrak,  Wakenya wengi walisema hawana pesa za kusherehekea.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved