Aliyekuwa mwanahabari mpekuzi na sasa ni mbunge wa eneo bunge la Nyali Mohamed Ali maarufu kama Jicho Pevu, ameweka wazi kwamba amefanyiwa upasuaji wa goti kutokana na jeraha alilolipata katika michezo iliyowaleta pamoja wabunge wa mataiafa ya jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mashindano hayo yalifanyika jijini Mombasa kwa takribani wiki mbili ambapo michezo mbali mbali ikiwemo soka, riadha, mpira wa vikapu na mchezo wa kuvuta kamba.
Kupitia ujumbe kwa anwani yake ya mtandao wa Instagram ,bunge huyo amesema kwamba upasuaji uliofanywa kwenye goti lake ulifanyika kwa mafanikio ila daktari wake alimweleza kuwa atapunguza kutembea kwa miezi mitatu ili apatge nafuu kamili.
Mbunge huyo ametangaza kuwa amesimamisha ratiba yake yote ya kisiasa wakati wa kuuguza majeraha ila amehakikishia wakaazi wa eneo bunge la Nyali kuwa shughu;li za ofisi yake zitafanyika bila kuhitilafiwa.
“Nina furaha kuwajulisha kuwa nimefanyiwa upasuaji wa goti vyema ila daktari wangu ameniambia nipunguze matembezi kwa angalau miezi mitatu kuhusu uponyaji kikamilifu.” Aliandika mbunge huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Jicho Pevu hata hivyo amewataka wananchi kumkumnbuka katika
maombi yao anapoendelea kupata nafuu akiahidi kuwa atarejea tena akiwa na nguvu
zaidi.